JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


 

  FEDHA NA UWAKALA

Huduma ya Fedha na Uwakala hufanyika kwa ajili ya wananchi kuwawezesha kupata huduma mbalimbali za kifedha na nyingine za aina hiyo zinazotolewa na Shirika kwa njia ya Uwakala. Huduma hizi ni kama ifuatavyo:

  1. Posta Keshi (Posta Cash)

Posta keshi ni jukwaa la upokeaji, usafirishaji na ulipaji wa fedha kutoka kwa mteja mmoja Kwenda kwa mwingine. Huduma hii hutolewa kwa wateja wa ndani ya nchi. Huduma hii ni miongoni mwa huduma zitolewazo kupitia katika mfumo wa Posta Kiganjani. Huduma hii ni ya gharama nafuu, hulipwa kupitia simu za mkononi, inaweza kupokelewa kwenye mtandao wowote wa simu, na mteja anaweza kutuma au kupokea fedha katika ofisi za Posta au kwa Wakala yeyote wa Posta aliyesajiliwa.

  1. Giro ya Posta (Post Giro)

Giro ya Posta ni huduma ya kulipa kwa niaba ya mteja. Mteja anaweza kutuma au kulipa au kupokea fedha kupitia mfumo huu wa malipo. Aidha, mteja anaweza kununua au kuuza hisa kupitia mfumo huu. Malipo yanayoweza kulipwa ni pamoja na:

 • Mafao ya uzeeni (pensheni),
 • Mishahara ya watumishi,
 • Ada za shule,
 • Kuuza na kununua hisa za makampuni yaliyosajiliwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam,
 • Mafao ya Bima,
 • Malipo ya gawio litokanalo na uwekezaji wa Hisa,
 • Kodi mbalimbali na
 • Ankara mbalimbali kama za maji na umeme.
  1. Huduma za Uwakala wa Fedha, Benki, Bima, Mitandao ya Simu na Ukataji tiketi za ndege

Huduma ya Uwakala imegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwemo kundi utumaji na Usafirishaji wa Fedha, kundi la Huduma za Mabenki, kundi la Bima na kundi la Huduma za Simu na kundi la Usafirishaji (ukataji tiketi za ndege kwa abiria).

 1. Usafirishaji Fedha: Shirika hupokea na kulipa wateja wake kupitia mifumo mbalimbali ya malipo ikiwemo Western Union, Money Gram kwa njia ya Uwakala
 2. Huduma za Mabenki: Shirika ni Wakala wa utoaji wa huduma za kibenki zikiwemo za Benki ya CRDB, TCB, NBC, PBZ na Equity Bank.
 3. Huduma za Bima: Shirika hutoa huduma za Bima kwa uwakala kwa NIC, ZIC na Assemble Insurance.
 4. Huduma za Simu: Shirika linatoa huduma mbalimbali za uwakala kwa Makampuni ya simu ya TTCL (T-Pesa), Vodacom (M-Pesa), Tigo (Tigo Pesa), na Halotel (Halo Pesa)
 5. Ukataji tiketi za ndege kwa wasafiri (Abiria): Shirika lina leseni ya kukata tiketi za makapuni mbalimbali ya ndege ndani na nje ya nchi kwa njia ya uwakala.

Mwananchi anaweza kukata tiketi ya ndege ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwenda mahali popote ndani na nje ya nchi. Leseni hii pia inaliruhusu Shirika kukata tiketi za mashirika mengine ya ndege kwa uwakala.

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA