TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19) NCHINI HUKU TUKIENDELEA KUWAHUDUMIA
Shirika la Posta Tanzania (TPC) linapenda kuwajulisha wateja wetu na umma kwa ujumla kuwa kufuatia maagizo na maelekezo ya Serikali ya kuwataka watanzania kuchukua tahadhari na
kujilinda dhidi ya kuenea kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19), Shirika kwa kulinda maslahi mapana na afya za wafanyakazi wake linapenda kupata ushirikiano kutoka kwa wateja wetu na umma kwa ujumla kwenye mambo yafuatayo:
- Kila mteja au mwananchi yeyote atakayefika kwenye ofisi za Posta popote nchini atalazimika kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka ama kupaka kitakasa mikono (sanitizer) zinazopatikana katika ofisi zetu mara anapoingia au kutoka baada ya kupatiwa huduma.
- Tunapenda kuwatangazia wateja wetu kuwa kama huna ulazima wa kufika ofisi za posta na unahitaji huduma zetu tafadhali wasiliana nasi kwa simu nambari 0738 070701. Taarifa zaidi kuhusu huduma zetu utazipata kupitia website yetu: www.posta.co.tz au mitandao yetu ya kijamii: twitter (posta_tz), facebook: (posta tanzania) na kupitia instagram: (posta_tz) kwa maelezo zaidi.
- Aidha tunawakumbusha wateja wetu kubaki nyumbani ili kupunguza maambukizi mapya zaidi ya virusi vya corona, na tunawasisitiza wateja wetu na watanzania kwa ujumla kufanya manunuzi ya bidhaa zao mbalimbali kupitia duka letu la mtandao kwa tovuti ifuatayo, www.postashoptz.postau piga nambari 0738 070701 na utafikishiwa bidhaa yako kwenye makazi yako au mahali ulipo.
Shirika linapenda kuwajulisha wateja wake na wananchi wote kwa ujumla kuwa bado tunatoa huduma hata wakati huu wa janga la Corona kwa kuwafikia pale watakapohitaji huduma zetu kwa mikoa yote ya Tanzania kupitia ofisi zetu.
Pia tunawajulisha kuwa ukihitaji huduma za kuchukua mizigo mteja alipo (pick up) au kukuletea (delivery) unaweza kutupata kupitia namba zilizoorodheshwa hapo chini, kwa mikoa yote nchini.
Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuliamini Shirika la Posta likuhudumie.
Imetolewa na:
Postamasta Mkuu
Shirika la Posta Tanzania
Makao Makuu, Dar es Salaam
NO. |
REGION |
PHONE NO |
NO. |
REGION |
PHONE NO |
1 |
REGIONAL MANAGER/ DSM |
0684 887 977 |
11 |
REGIONAL MANAGER/ MOROGORO |
0684 887 850 |
DSM EMS OFFICE |
0684 887 972 |
MOROGORO EMS OFFICE |
0684 887 851 |
||
2 |
REGIONAL MANAGER/ ARUSHA |
0684 887 769 |
12 |
REGIONAL MANAGER/ KILIMANJARO |
0684 887 866 |
ARUSHA EMS OFFICE |
0684 887 767 |
KILI'NJARO EMS OFFICE |
0684 887 858 |
||
3 |
REGIONAL MANAGER/KAGERA |
0684 887 770 |
13 |
REGIONAL MANAGER/ MTWARA |
0684 887 869 |
KAGERA EMS OFFICE |
0684 887 778 |
MTWARA EMS OFFICE |
0684 887 874 |
||
4 |
REGIONAL MANAGER/ MWANZA |
0684 887 886 |
14 |
REGIONAL MANAGER/ MBEYA |
0684 887 836 |
MWANZA EMS OFFICE |
0684 887 887 |
MBEYA EMS OFFICE |
0684 887 826 |
||
5 |
REGIONAL MANAGER/ RUVUMA |
0684 887 888 |
15 |
REGIONAL MANAGER/ LINDI |
0684 887 819 |
RUVUMA EMS OFFICE |
0684 887 509 |
LINDI EMS OFFICE |
0684 887 816 |
||
6 |
REGIONAL MANAGER / SHINYANGA |
0684 887 904 |
16 |
REGIONAL MANAGER/ MUSOMA |
0684 887 985 |
SHINYANGA EMS OFFICE |
0684 887 548 |
MUSOMA EMS OFFICE |
0684 887 820 |
||
7 |
REGIONAL MANAGER/ SINGIDA |
0684 887 986 |
17 |
REGIONAL MANAGER/ RUKWA |
0684 887 940 |
SINGIDA EMS OFFICE |
0684 887 906 |
RUKWA EMS OFFICE |
0684 887 940 |
||
8 |
REGIONAL MANAGER/ TABORA |
0684 887 798 |
18 |
REGIONAL MANAGER/ ZANZIBAR |
0684 887 935 |
TABORA EMS OFFICE |
0684 887 918 |
ZANZIBAR EMS OFFICE |
0684 887 549 |
||
9 |
REGIONAL MANAGER/ TANGA |
0684 887 991 |
19 |
REGIONAL MANAGER / KIGOMA |
0684 887 533 |
TANGA EMS OFFICE |
0684 887 919 |
KIGOMA EMS OFFICE |
0684 887 812 |
||
10 |
REGIONAL MANAGER/ DODOMA |
0684 887 810 |
20 |
REGIONAL MANAGER/ IRINGA |
0684 887 949 |
DODOMA EMS OFFICE |
0686 887 348 |
IRINGA EMS OFFICE |
0684 887 941 |
||
MANAGER /EMS HQ |
0684 973 837 |
GENERAL MANAGERS BUSSINESS OPERATIONS |
0684 887 952 |
||
WEBSITE: www.posta.co.tz |