SHINDA ZAWADI MBALIMBALI NA SHIRIKA LA POSTA

        LOGO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA                        TPC LOGO

WIZARA YA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI

 

 

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

 

 

SHINDA ZAWADI MBALIMBALI KWA KUSHIRIKI MASHINDANO MAALUMU YA UANDISHI WA BARUA, MAKALA, INSHA, UBUNIFU BORA WA VIBONZO (MOVING GRAPHICS)  NA TEHAMA KWA MWAKA 2021.
 
 
Shirika la Posta Tanzania linapenda kuwakaribisha wanafunzi, waandishi wa habari, wasanii, wanamichezo, wabunifu bora wa vibonzo/graphics na wabunifu wa mifumo ya TEHAMA kushiriki katika mashindano yafuatayo;-
 
 
1.   UANDISHI WA BARUA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WENYE UMRI USIOZIDI MIAKA 18. 
 
Mada:-  “Barua ya ushawishi kwa rafiki yako atumie huduma mpya  za kidijitali za Shirika la Posta Tanzania kwa manufaa yake binafsi na kwa mendeleo ya Taifa”
 
 
 
2.  UANDISHI WA INSHA KWA WANAMICHEZO NA WASANII. 
 
Mada:-  “Mabadiliko ya teknolojia kwa maendeleo ya Posta”.
 
 
 
3.  UANDISHI WA MAKALA KWA WANAHABARI.
 
Mada:-  “Mchango wa huduma za kidijitali za Posta katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania”.  
 
 
 
4.  UBUNIFU WA VIDEO INAYOTUMIA VIBONZO(MOVING GRAPHICS) BORA KUTOKA KWA WABUNIFU WA VIBONZO(MOVING GRAPHICS) HAPA NCHINI.
 
Mada:- Ionyeshe “Huduma za Posta zinavyochukua fursa katika mabadiliko ya kiteknolojia”.
 
 
 
5.  WABUNIFU WA MIFUMO YA TEHAMA (ICT) KATIKA MAWASILIANO YA POSTA.
 
Mada:- “Kutengeneza wazo (Concept) ya mifumo itakayotoa suluhisho kwa changamoto za mawasiliano ya Posta Tanzania”
 
 
 
Masharti Muhimu:-
UREFU:  Barua: Maneno kati ya 500 hadi 1000.
 
MAKALA:  Maneno kati ya 1500 hadi 2000.
INSHA:  Maneno kati ya 1000 hadi 2000.
VIDEO YA VIBONZO/GRAPHICS:  dakika 5 hadi 10
UBUNIFU WA TEHAMA: Katika kurasa zisizozidi 6
 
LUGHA:- Tumia Kiswahili kwa uandishi wa makala , insha, ubunifu wa vibonzo na TEHAMA.      
 
Kiswahili/Kiingereza:  Kwenye uandishi wa Barua pekee. 
 
 
JINSI YA KUTUMA NA KUSHIRIKI:
 
Shindano la Barua :- Mashindano haya yanapokelewa kwa njia ya barua ya kawaida ziazotumia stempu. Kila barua iwekwe katika bahasha yake. 
 
Shindano la Makala, Insha, Ubunifu wa Graphic na mifumo ya TEHAMA:- 
 
Mashindano haya yanapokelewa kwa njia EMS.
 
Kila mshiriki azingatie kuandika anwani yake kwa usahihi na ataje utambulisho zaidi ikiwemo Jina Kamili, Umri, Jinsia Na Shule/Chombo Cha Habari Anachotoka na atume kwenda anuani ifuatayo:-
 
 
IDARA YA MASOKO,
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA,
7 MTAA WA GHANA,
S. L. P 9551, 11300 DAR ES SALAAM
 
Mwisho wa kupokea mashindano haya ni tarehe 20 Septemba, 2021.
 
Tafadhali uonapo tangazo hili uwajulishe wanafunzi/waandishi wa makala/wadau walio karibu nawe ili wapate kushiriki mashindano haya na kujinyakulia zawadi nono kama vile Komputa mpakato (Laptops), Runinga, Camera, simu za mikononi, vifaa vya shule kwa wanafunzi, pesa taslimu na nyinginezo nyingi.
 
Mshindi wa 1 hadi 3 kwenye kila shindano atapata nafasi ya kukabidhiwa zawadi yake siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta duniani tarehe 9 Oktoba, 2021.
 
 
 
“Posta ni zaidi ya Barua”
 
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!