pCUM

1.0: Barua Za Dharura Mijini (pCUM)

pCUM  ni huduma ya kusafirisha vifurushi ndani ya jiji/mji kwa dharura, kwa uhakika  na kwa bei nafuu inayotolewa na Shirika la Posta Tanzania. Ni njia yenye manufaa yanayolingana na gharama na yenye ufanisi katika kuwasilisha nyaraka na vifurushi ndani ya jiji/mji.

2.0: FAIDA ZA pCUM

2.0.1: Haina usumbufu na ni ya uhakika na inakusudia kurahisisha usambazaji wa nyaraka na vifurushi ndani ya ofisi hususan kwa shirika lenye kiasi kikubwa cha mizigo ya kusambaza ndani ya mji huohuo.

2.0.2: Inatoa kiwango cha juu cha huduma kwa wateja kitaalam kwa njia ya kumfikia mtu mmoja mmoja na kama njia ya kuifikia familia.

2.0.3: Inatoa huduma ya kuchukua na kufikisha huduma mahali popote pale ndani ya mji.

2.0.4: Ni shughuli ya kuchukua na kupeleka nyaraka na vifurushi kwa wakati; hivyo inaongeza kuridhika kwa wateja.

2.0.5: Inawapunguzia Wateja usumbufu unaohusishwa na kwenda Ofisi ya Posta, kubandika stempu za kuposti au barua zinazotumwa bila malipo.

2.0.6: Kupata usafiri, upokeaji na utambuaji mzuri wa vifaa ni sifa ya muhimu ya pCUM

2.0.7: Inaendeshwa kwa uzoefu na wafanyakazi wanaojali mteja  

Tazama Bei za Pcum

Tanzania Census 2022

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!