AINA ZA HUDUMA ZA BARUA ZA HARAKA (EMS)

1.  Ufikishaji wa Nyaraka na Vifurushi kwa EMS:

Uwezo wa EMS: Mahitaji ya sekta nzuri, ya haraka ya biashara yamesababisha kuanzishwa kwa huduma za haraka za EMS.  Lakini ilikuwa ni huduma ya utaalamu wetu, iliyofanywa kama ya binafsi na msisitizo wetu katika kutoa huduma bora kwa mteja ndiyo uliyoifanya huduma ya EMS kuaminika na kuwa na idadi kubwa ya ongezeko la wateja!

Huduma za EMS zinatolewa kwa wakati na kwa uhakika Tanzania nzima, Afrika Mashariki na duniani kote.  Tunaunganisha ndege kadhaa na kufuatilia nyaraka au mzigo wako kwa kompyuta!

HUDUMA ZA NDANI: Utoaji wa huduma siku inayofuata ni wa uhakika katika vituo vingi na siku ya tatu kwa vituo vilivyobaki kwenye maeneo ya vijijini.

KUBEBEWA BURE! Kwa wateja wetu wa kawaida, kwa kupiga simu wakala wetu wa EMS atakuja kuchukua nyaraka au mizigo yako nyumbani au ofisini kwako.

HUDUMA ZA KIMATAIFA: Muda wa kufikisha unatofautiana kati ya siku mbili hadi tano kulingana na eneo mzigo unakokwenda na ucheleweshaji/usumbufu wa ndege. Unapohitaji kutuma mzigo nje ya nchi huduma ya Kimataifa ya EMS ni suluhisho lako.

Nchini Uingereza huduma ya EMS inajulikana kama DATAPOST; Ufaransa kama CHRONOPOST; India kama SPEEDPOST; na Marekani, Ujerumani na Japani kama EMS: Huduma inayoongoza duniani kwa usalama na uharaka.

 Ili kurahisisha biashara yako au mahitaji ya haraka ya usafirishaji, unaweza kuanzisha akaunti ya mkopo kwa ajili ya biashara ya ndani au ya kimataifa kwa EMS ili uweze “kuagiza sasa na kulipa baadaye!” Tafadhali mwone wakala wa EMS aliye jirani nawe kwa ajili ya kupata taarifa zaidi!

2. FAKSI KWA EMS

 Ujumbe wa haraka kwa mteja, rafiki au mwanafamilia wa nchini, katika kanda au wa kimataifa? Tuma faksi kwa EMS na kuwa na uhakika ujumbe wako umetumwa ndani ya saa 24 kwa mtu au kampuni inayohusika! Ujumbe, grafiki, majedwali, picha, michoro: Faksi kwa EMS inaweza kutuma nyaraka zote hizi iwe zinatumwa nchini au kokote duniani. Nakala ya ujumbe usio wa rangi (yaani nyeusi na nyeupe) inayoonekana vyema itatumwa kwenye anwani ya faksi yako ya biashara au makazi.

 Je, huna kipepesi/mashine ya nukushi? Hakuna tatizo! Faksi itatumwa kwenye anwani ya ofisi ya EMS iliyo karibu nawe na Ofisi ya EMS itakupigia simu ili kukufahamisha kwamba ujumbe umetumwa na unaweza kuchukuliwa katika ofisi ya EMS.

 

Tanzania Census 2022

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!