Posta Mlangoni
1.0: Posta Mlangoni (pM)
pM ni huduma ya haraka na ya uhakika na ya gharama nafuu inayotolewa na Shirika la Posta Tanzania ndani ya jiji/mji. Ni njia ya gahrama nafuu na yenye ufanisi katika kutuma nyaraka na vifurushi ndani ya jiji/nchi
2.0: MANUFAA ya Posta Mlangoni
2.0.1: Haina usumbufu na ni ya uhakika na imeandaliwa kwa ajili ya kutuma nyaraka na vifurushi baina ya ofisi hasa kwa taasisi zinazotuma nyaraka nyingi ndani ya mji mmoja.
2.0.2: Inatoa kiwango cha juu cha huduma kwa wateja kwa utaalamu kwa kila mtu kama familia
2.0.3: Inatoa huduma ya kuchukua na kupeleka mizigo nyumba kwa nyumba popote pale ndani ya mji mmoja
2.0.4: Nyaraka na vifurushi vinapatikana kwa muda mwafaka; hivyo inaongeza kuridhika kwa wateja.
2.0.5: Inawapunguzia Wateja usumbufu unaohusishwa na kwenda Ofisi ya Posta, kubandika stempu kwa ajili ya utumaji s2au barua zinazotumwa bila malipo.
2.0.6: Usalama katika usafirishaji, ufikishaji na usimamizi mzuri wa nyaraka ni sifa muhimu za Posta Mlangoni.
2.0.7: Inaendeshwa na wafanyakazi wenye uzoefu na wanaojali wateja.
Tazama Bei za Posta Mlangoni