Huduma za Kifedha

Maduka ya kubadilishia fedha.

Vituo vya kubadilishia fedha vya Posta, vinatoa huduma za kubadilisha sarafu na noti za kigeni kwa viwango vizuri ukilinganishwa na maduka mengine ya kubadilishia fedha Nchini. Mpaka sasa TPC ina maduka 26 za kubadilishia fedha kote Nchini.

Uwakala wa kifedha.

Huduma hizi zinatolewa kwa njia ya mtandao wa posta kwa kuzingatia makubaliano kati ya TPC na Taasisi nyinginezo. Kupitia ofisi za Posta, Shirika linatoa huduma za kifedha kama vile Western union, huduma za ATM, na kutuma pesa kupitia T-Pesa (TTCL), huduma za miamala ya kifedha kupitia Benki mbalimbali kama CRDB, Benki ya TCB, Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), NBC, ATCL na kutoa huduma za Kiserikali kuptia vituo vya HUDUMA PAMOJA.

Steshenari na maduka ya intaneti

Wateja wanapata huduma nafuu za Intaneti, vifaa vya kiofisi na mashuleni kupitia maduka ya shirika la Posta yaliyoko kwenye ofisi za Posta za Wilaya kote Nchi Nzima.

 

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!