Kuhusu Shirika la Posta Tanzania

 Shirika la Posta Tanzania (TPC) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 19 ya mwaka 1993 na kuanza rasmi kutoa huduma zake mnamo tarehe 1 Januari, 1994 likiwa na jukumu la kutoa huduma za ndani za kiposta na huduma za posta za kimataifa. 

Shirika liko chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambayo ina jukumu la kusimamia, kutunga sheria, sera na miongozo mbalimbali kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika.

 

 Huduma/Biashara zitolewazo na Shirika ni pamoja na:

 

1. Huduma ya usafirishaji wa Barua, nyaraka, vifurushi, vipeto na mizigo mikubwa kupitia njia ya kawaida.

 

2. Huduma ya usafirishaji wa Barua, nyaraka, vifurushi, vipeto na mizigo mikubwa kupitia njia ya Haraka (EMS)

 

3. Usafirishaji wa mizigo hadi tani 30.

 

4. Huduma za uwakala wa kifedha. 

 

5. Huduma za Biashara mtandao kupitia (posta e-shop,philatelic e-shops). 

 

6.Huduma za kiserikali kupitia vituo vya Huduma Pamoja.

 

7. Huduma zingine za rejareja zinazojumuisha uuzaji wa vifaa vya kuandikiavifaa vya matumizi ya Ofisi na Shule.

 

8. Huduma za intaneti kupitia vituo vya Inteneti vya Posta.

 

Kutoa huduma bora za Posta, Usafirishaji, Fedha, Biashara Mtandao na huduma za Kiserikali zinazokidhi matakwa ya wadau.

Mtoa huduma za Posta bunifu na uhakika zinazoendana na vionjo vya wateja katika uchumi wa kidijitali.

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!