Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Posta inatoa huduma za posta kitaifa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ni kiungo muhimu cha huduma za usafirishaji kati ya Tanzania na dunia.

Huduma za usafirishaji wa Barua na Vifurushi, Usafirishaji wa Mizigo kwa Haraka, Fedha na Uwakala, huduma za kutumia TEHAMA, pamoja na usanifu, kufunga na kukodi masanduku na mabegi ya kupelekea barua binafsi, uzalishaji na mauzo ya bidhaa za stempu na huduma nyingine ndogo ndogo ambazo zinajumuisha uuzaji wa viandikia na vifaa kwa ajili ya matumizi ya ofisi na shule.

Ni huduma ya usafirishaji wa haraka wa barua, nyaraka na vifurushi ambapo mteja hulipa gharama zaidi za usafirishaji kutumia huduma hii.

Bei za huduma zetu zinatofautiana katika namna nyingi. Tazama bei katika sehemu ya orodha ya bei kwenye tovuti au bofya kiungo https://posta.co.tz/index.php/tariffs

 

OFISI YA POSTAMASTA MKUU

MAKAO MAKUU YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Mtaa wa 7 Ghana,

S.L.P 9551

11300, Dar es Salaam

TelegramU: POSTGEN

Faksi (022) 2113081

Mobile: +255684887551

Barua Pepe: pmg@posta.co.tz

Tovuti: www.posta.co.tz 

 

Ofisi za Posta zipo katika mikoa yote, unaweza kuwasiliana kupitia kiungo hiki: https://posta.co.tz/index.php/contact-us

Hii ni biashara ya mtandaoni ya kuuza na kununua vitu kupitia duka mtandao la Shirika la Posta.  Tembelea link ifuatayo kwa maelezo zaidi: https://www.postashoptz.post/

Ndiyo, na ni rahisi, mtu anaweza kuomba sanduku kwa njia ya mtandao, bofya kiungo hiki https://smartposta.posta.co.tz/  Jaza taarifa zinazotakiwa na ufuate maelekezo.

Ni huduma ya kusafirisha barua, vifurushi na nyaraka kwa gharama nafuu na kumfikishia mteja hadi mahali alipo kupitia anwani za makazi na Postikodi.

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!