Posta Yaingia Mkataba Na NBC Kutoa Huduma Za Kibenki

05 October 2019

Shirika la Posta Tanzania na Benki ya NBC leo tarehe 18 Septemba, 2019, wamesaini mkataba wa kibiashara utakaowezesha kutoa huduma za kibenki kupitia matawi ya Shirika la Posta Tanzania.

postanbc

Postamasta Mkuu Bw. Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NBC Bw. Theobald Sabi wakibadilishana hati ya makubaliano ya kibiashara baada ya kutiliana saini.

Tukio hilo la utiaji saini wa mkataba huo liliambatana na uzinduzi wa huduma ya uwakala kupitia kaunta rasmi ya NBC iliyoko Posta kuu jijini Dar es Salaam (GPO), ambayo imeanza rasmi kutoa huduma hizo za kibenki. Hafla za uzinduzi huo ilifanyika katika eneo la ofisi za Posta Mpya (GPO) jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali ikiwemo mkurugenzi Usimamizi wa sekta ya fedha wa Benki kuu Bw. Jerry Wambura Sabi, wadau wa bishara na maofisa kutoka Shirika la Posta na NBC

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mh. Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (Mb). Akizungumza baada uzinduzi huo Mh. Waziri amelipongeza Shirika la Posta kwa juhudi zake za kuwakaribisha wadau mbalimbali ili waweze kulitumia ili kutoa huduma zao nchi nzima, na vilevile aliipongeza benki ya NBC kwa utendaji wake hata kutoa gawio kwa serikali.

Aidha Mh. Kamwelwe ameongezea kuwa,makubaliana hayo yataleta tija kwa serikali na maendeleo ya nchi kwa ujumla na anaamini kwamba utaleta manufaa makubwa sana kwa pande zote mbili.

 

 

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!