SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAFANYA KIKAO KIKUU CHA PILI CHA MWAKA NA KUELEZA MAFANIKIO NA MATARAJIO YA KWA MWAKA 2019/2020

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania , mara baada ya mkutano huo. Kulia waliokaa ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bibi Kitolina Kippa na Mwakilishi wa Msajili wa Hazina, Bw. Elikana Mtumweni. Aliyesimama kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TCRA), Bw. Wilfred Maro.

Tarehe 17 Juni, 2020 Shirika la Posta Tanzania limefanya Mkutano Mkuu wa pili wa mwaka (2nd ANNUAL GENERAL MEETING), Uliofanyika Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, Jijini Dar es Salaam, kueleza Mafanikio na matarajio ya Shirika pamoja na mchango wake kwa jamii na Serikali.

Tukio hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu Dkt Haruni Kondo amewataka wafanyakazi kuchapa kazi  sambamba na mabadiliko ya Sayansi na Tekinolojia ili kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi ndani ya Shirika.

Mwenyekiti ameelezea jinsi Shirika lilivyotumia ukubwa na Upana wa mtandao wake kujiendesha kibiashara na kupata faida na hatimaye kuweza kuongeza mishahara ya wafanyakazi kitu ambacho kimeleta hamasa kwa wafanyakazi hata kuongeza tija.

Aidha Mwenyekiti ameeleza jinsi Shirika la Posta Tanzania linavyojikita katika kutoa huduma ya Posta Mlangoni huku akisisitiza kuwa huduma hiyo inakawia kutokana mfumo wa anwani za makazi na Postikodi kutokamilika kwa kuwa huo ndiyo muundombinu wa kutekeleza kwa ukamilifu huduma hii ya posta mlangoni.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ameeleza azma ya Shirika la Posta Tanzania kutoa gawio kwa Serikali lililotokana na faida ambayo imepatikana kwa kipindi cha mwaka 2018/2019.

Imetolewa na Kitengo cha Mahusiano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!