SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAENDESHA MAFUNZO YA NDANI KUBORESHA HUDUMA ZA EMS KIDIGITALI.

Leo Tarehe 24 mwezi Juni 2020, Shirika la Posta Tanzania limeendesha Mafunzo kwa baadhi ya wasimamizi na Maofisa wa Idara ya EMS ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi kwenye idara ya hiyo, kipindi hiki ambacho, Shirika linafanya mageuzi mbalimbali ya kutoa huduma zake kwa njia ya kidigitali.
 
Mafunzo hayo yalitolewa Kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, Jijini Dar es Salaam na Meneja Tehama (ICT) wa Shirika hilo, Insp. Reuben Komba. Meneja huyo alifundisha namna Mifumo hiyo mipya itakavyofanya kazi na ufanisi wake kwenye kupokea na kutuma mizigo kwa njia ya EMS. 
 
Aidha Insp Komba alieleza mafanikio yatakayopatikana kupitia mfumo huo ndani ya Shirika, na kwamba moja ya mafanikio hayo ni kuleta chachu ya kupata Biashara mpya ndani ya huduma za EMS.
 
Akizungumza katika mafunzo hayo Insp Komba aliongeza kuwa EMS itakuwa na uwezo wa kupokea wateja wanaolipa hapohapo (Cash pay) na wateja wa malimbikizo (Billing pay), Ambapo pia alieleza kuwa EMS iandae utaratibu wa kuwa na account kwa wateja wa ‘Corparate’ na wale wa ‘Regional’ ili kuweka urahisi wa wateja hao kufwatilia kwa karibu mwenendo wa vifurushi vyao.
 
Mafunzo hayo mbali na kuhudhuriwa na maofisa kutoka idara ya EMS pia yalihudhuriwa na Meneja EMS ndugu Mbarouk Issa Sasilo, pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa idara ya TEHAMA (ICT).
 
 
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO 
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!