KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI UCHUKUZI NA MAWASILIANO (SEKTA YA MAWASILIANO) AZIKUMBUSHA TAASISI ZA SERIKALI KUTUMIA HUDUMA ZA POSTA KUSAFIRISHA BIDHAA NA VIFURUSHI KWA USALAMA ZAIDI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainab Chaula amezikumbusha Taasisi za Serikali kutumia huduma za Shirika la Posta Tanzania (TPC) kusafirisha bidhaa, vifurushi na vipeto kwa usalama zaidi.

Dkt. Chaula alisema kuwa TPC imepewa dhamana kisheria kuwa msafirishaji mkuu wa barua, vifurushi, vipeto na bidhaa mbali mbali kwa mujibu wa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 19 ya mwaka 1993 iliyoanzisha Shirika hilo nani Shirika la umma ambapo Serikali imewekeza.

Ameitaka TPC kuunganisha huduma za posta na anwani za makazi na Postikodi na simu za mkononi ili kuhudumia wananchi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kurahisisha na kufanikisha usambazaji na usafirishaji wa barua, vifurushi, vipeto na bidhaa kwa wananchi.

Naye Posta Masta Mkuu wa TPC, Bwana Hassan Mwang’ombe ameziomba taasisi za Serikali kutumia Shirika hilo kusafirisha barua, vifurushi na vipeto kwa kuwa bidhaa zao zitafika kwa usalama na uhakika kwa kuwa Shirika hilo linatumia huduma ya mtandao wa TEHAMA kutoa huduma zake kwa wateja kwa kuunganisha ofisi zake 202 zilizopo maeneo mbali mbali nchi nzima; wana wataalamu wa lojistiksi; na wanatumia anwani za makazi na postikodi kuhudumia wateja.

Naye Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika hilo, Mwanaisha Ally Said, ameiomba Wizara kuhakikisha kuwa watoa huduma za usafirishaji wa nyaraka, vifurushi na vipeto wasio na leseni ya kuendesha biashara hiyo inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ili kuhakiisha kuwa wananchi wanapata huduma za sekta ndogo ya posta na Serikali inapata mapato yake.
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!