TAARIFA KWA UMMA, MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA SABASABA

Shirika la Posta Tanzania (Posta) linapenda kuwakaribisha wananchi wote kutembelea jengo la Posta ndani ya viwanja vya maonesho ya 44 ya kimataifa ya biashara, maarufu kama SABASABA.
 
Maonesha ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya "Uchumi wa viwanda kwa ajira na biashara endelevu" yanaanza rasmi tarehe 1 Julai 2020, huku Posta ikiwa imejipanga kutoa huduma za kubadilisha fedha, sanduku la barua kiganjani "Smart Posta", huduma za 'stationery', biashara ya duka la mtandao, na maelezo kuhusu huduma zetu mbalimbali zilizoboreshwa kwenye mifumo ya kidigiti.
 
Kwa watakaofika viwanja vya maonesho ya sabasaba, jengo la Posta lipo barabara ya kwanza kushoto ukitokea geti kuu la kuingia kwenye viwanja vya maonesho, aidha jengo letu linatazamana na jengo la Shirika la Reli Tanzania (TRL).
 
Tunawakaribisha watu wote kutembelea jengo la Posta kujionea huduma mbalimbali zilizoboreshwa ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa sambasamba na wateja wetu.
 
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
Shirika la Posta Tanzania.
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!