WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA BANDA LA POSTA NDANI YA VIWANJA VYA MAONESHO YA SABASABA.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa(MB) ametembelea Jengo la Shirika la Posta lililopo ndani ya viwanja vya maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara, maarufu kama 'Sabasaba' na kujionea huduma mbalimbali  zinazotolewa na Shirika hasa kwenye kipindi hiki ambapo Shirika limefanya mabadiliko makubwa ya utoaji huduma yanayozingatia matakwa ya wateja na hali ya soko.
 
Mheshimiwa Bashungwa ameeleza kufurahishwa kwake na mafanikio ambayo Posta imeyafikia katika kutoa huduma zake hasa kipindi hiki cha mabadiliko ya Sayansi na Tekinolojia. Sambamba na hilo Mheshimiwa waziri  alipata maelezo mafupi kuhusu huduma mpya ya "POSTA KIGANJANI" 
 
Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya "Uchumi wa viwanda kwa ajira na biashara endelevu" yameanza rasmi tarehe 1 Julai 2020, huku Posta ikiwa imejipanga kutoa huduma za kubadilisha fedha, sanduku la barua kiganjani "Smart Posta", huduma za 'stationery', biashara ya duka mtandao, na maelezo kuhusu huduma mbalimbali zilizoboreshwa kwenye mifumo ya kidigiti.
 
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano 
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!