NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (SEKTA YA MAWASILIANO) DR. JIM YONAZI, AFUNGUA KIKAO KAZI CHA IDARA YA MASOKO KATIKA MAKAO MAKUU YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

Tarehe 5 Oktoba, 2020 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dr. Jim Yonazi amefungua kikao kazi cha Maafisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania. 

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya Makao Makuu ya Shirika hilo kililenga kujadili mbinu na mikakati ya kibiashara na masoko ndani ya Shirika, Umuhimu wa Ushirikiano baina ya Idara ya Masoko na Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Shirika, na namna ya kufanya masoko kwa kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Aidha semina elekezi hiyo ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Mhandisi Clarence Ichwekeleza na Mkufunzi Nguli wa Masuala ya Habari na Mawasiliano Nchini, Bwana Innocent Mungi.

Semina elekezi hiyo ilimalizika tarehe 6 Oktoba 2020.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

 

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!