SAJILI NAMBA YAKO YA SIMU KUWA SANDUKU LAKO LA BARUA.

Shirika la Posta Tanzania linawakaribisha wateja wetu na watanzania kwa ujumla kujiunga na kutumia huduma yetu mpya ya Posta kiganjani,

2.0 POSTA KIGANJANI NI NINI,
Posta kiganjani ni sanduku la Barua linalotumia simu janja (smart phone) ya kiganjani.

Namba ya simu ya mteja ndio itakayosajiliwa kama sanduku lake la barua (virtual Box). Wateja binafsi watatumia nambari zao binafsi za simu kujisajili, huku wateja wa Makampuni na Mashirika watatumia nambari ya Kampuni au Shirika husika kufanya usajili wa huduma za Posta Kiganjani.

Wateja wetu waliosajiliwa watakuwa na uwezo wa kufuatilia barua na vifurushi vyao na kujua ni wapi vimefika kupitia simu zao za mkononi. Mteja atajulishwa kwa ujumbe mfupi ‘sms’ ikimtaarifu kufika kwa kifurushi chake, ambapo atakuwa na haki ya kuamua apelekewe mahali alipo au afuate katika ofisi ya Posta iliyo karibu nae. Endapo mteja atachagua kupelekewa mzigo wake mahali alipo basi atachangia gharama kidogo kwa ajili ya ufikishwaji wa kifurushi au barua yake.

3.3 HATUA ZA KUJISAJILI,

Mteja atajisajili kupitia tovuti ya Shirika la Posta ambayo ni www.posta.co.tz au smartposta.posta.co.tz kisha atajaza taarifa zake na namba za simu, baada ya hapo atapokea ujumbe mfupi ukimtaarifu kuwa amefanikiwa kujisajili kwenye huduma ya Posta Kiganjani.

3.4 GHARAMA ZA MTUMIAJI WA HUDUMA YA POSTA KIGANJANI,

Baada ya kukamilisha usajili mteja atatumiwa ‘control number’ . Kwa wateja binafsi watalipia shilingi 14,160/= kutumia huduma kwa mwaka, huku wateja wa Mashirika na Makampuni watalipia 59,000/= kwa mwaka.

 

3.5 FAIDA YA POSTA KIGANJANI KWA JAMII

    Huduma hii inaokoa muda wako wewe mteja wetu na kuepusha kabisa usumbufu wa kufika mara kwa mara kwenye ofisi za Posta kuangalia kila mara kama barua yako au kifurushi chako kama kimefika.
    Mteja atakuwa na uwezo wakati wowote mahali popote alipo kwa kutumia simu yake ya mkononi kufuatilia na kujua mahali barua/kifurushi chake kilipofikia, hivyo inampa mteja uhakika wa kujua ni wakati gani aende kuchukua au kuletewa barua/ kifurushi chake bila kubahatisha.
    Inampa mteja uhakika wa kupata barua na kifurushi chake kwa wakati.
    Inampa mteja urahisi wa kulipia huduma za Posta kupitia simu yake ya mkononi.
    Inampa mteja uhuru wa kuandika ama kutokuandika jina la mpokeaji, (Namba ya simu itatumika kama kitambulisho).
    Mteja ana uwezo kuomba kuletwa huduma za posta mpaka mlangoni kwake kwa gharama nafuu za ziada.

Posta tunakwenda kidigitali!!!

Karibu Posta tukuhudumie.IMG 20210301 WA0006

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!