POSTA BORESHENI MIFUMO YA SHIRIKA, DKT NDUGULILE.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(MB) amelitaka Shirika la Posta Tanzania, kuboresha mifumo ya uendeshaji wa Shirika ili kuhakikisha kuwa mifumo ya TEHAMA inayotoa huduma kwa wateja inaendana na kufuata taratibu kuanzia mteja anapowasilisha barua yake, kifurushi au huduma nyingine yoyote mpaka hatua ya kulipia na kuweka kumbukumbu za huduma iliyotolewa kwa njia ya kielektroniki. Badala ya sasa ambapo huduma hizo zinafanyika kwa mtindo wa zamani kwa kuandika kwenye karatasi na kila kitengo kufanya kazi kivyake bila muingiliano wa mifumo katika utaratibu wenye mtiririko maalumu.
 

Dkt Ndugulile ameyasema hayo tarehe 16 Machi 2021, wakati wa ziara yake Mkoani Arusha alipotembelea Ofisi za Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kukagua utendaji kazi wa taasisi hizo mkoani humo baada yakufikisha siku 100 tangu kuundwa kwa Wizara hiyo mpya.


Naye, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Bwana Hassan Mwang’ombe, amemshukuru Dkt. Ndugulile kwa ziara hiyo na kuahidi kuwa watafanikisha maboresho hayo ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhudumia wananchi kwa mtazamo mpya na utendaji mpya unaoendana na kasi ya teknolojia.
 
Dkt. Ndugulile anaendelea na ziara yake mkoani Arusha ya kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Wizara na taasisi zake pamoja na kuhabarisha umma mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 tangu kuundwa kwa Wizara hiyo mwezi Disemba mwaka jana.

 

IMG 20210317 WA0004

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(MB) akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (hawapo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Arusha. Kushoto anayesikiliza ni Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Bwana Hassan Mwang’ombe

IMG 20210317 WA0009

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania Mkoani Arusha wakati wa ziara yake. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Mhandisi Clarence Ichwekeleza na wa kwanza kushoto ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Bwana Hassan Mwang’ombe

 IMG 20210317 WA0008

 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoani Arusha wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi wa Shirika hilo.

 

BeautyPlus 20210317123713318 save

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoani Arusha wakikwa kwenye picha ya pamoja.

 

Na Rachel Kitinya

KITENGO CHA MAWASILIANO

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

 

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!