POSTA YAENDESHA SEMINA ELEKEZI YA UONGOZI.

POSTA YAENDESHA SEMINA ELEKEZI YA UONGOZI.
 
 
IMG 194911
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo (Aliesimama Katikati), akitoa mwelekeo wa Shirika wakati wa "semina elekezi" kwa Viongozi Waandamizi  na Viongozi Waandamizi Wakuu"Principals and Senior Officers" wa Shirika la Posta Tanzania katika ukumbi wa NSSF Posta Azikiwe, tarehe 29 Mei 2021, kulia ni Mkufunzi mbobezi wa masuala ya uongozi kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (Institute of Directors Tanzania)  Bw. Andulile Mwakalyelye.
 
 
Na Rachel Kitinya.
 
Tarehe 29 Mei 2021 Shirika la Posta Tanzania limeendesha semina elekezi ya uongozi kwa viongozi waandamizi wakuu na viongozi waandamizi Daraja la kwanza ( I ) na Daraja la pili (II), Semina hiyo imefanyikia katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la NSSF Azikiwe Posta Jijini Dar es Salaam, ikiwa na  lengo la  kuwajengea uwezo viongozi waandamizi wa Shirika hilo ili kuwawezesha kumudu majukumu yao.
 
Semina hiyo Elekezi imeendeshwa na *Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania* (Institute of Directors Tanzania) chini ya mkufunzi mbobezi wa masuala ya uongozi, Bw. Andulile Mwakalyelye.
 
Akifungua semina hiyo Kaimu PostaMasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Daniel Mbodo, alieleza mwelekeo wa Shirika na kusisitiza kuwa, ili kufikia malengo ya Shirika kama yalivyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa saba wa Shirika (2019/2020 - 2023/2024) ikiwemo kulifanya Shirika la kidijitali, vipaumbele vitatu vitazingatiwa na kupewa uzito stahiki;
1. Mikakati ya kuongeza Mapato
 
2. Mikakati ya kupunguza na kubana Matumizi.
 
3. Kuongeza kasi ya utendaji kazi na kuachana na utendaji kazi wa mazoea huku teknolojia ikitumika kama "game changer"
 
Aidha, Kaimu Postamasta Mkuu amewaeleza viongozi hawa walioshiriki wapatao 150 kuwa ana imani kubwa na wao na kuwa wakitimiza wajibu wao kwa kuzingatia vipaumbele hivyo vitatu kwa kuwaongoza watendaji walio chini yao, kutoa ushirikiano na kuwashauri vyema viongozi walioko juu yao, Malengo ya Shirika na maono ya Shirika yatatimiza matarajio ya Serikali.
 
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano.
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
 
 
 
ZIFUATAZO NI PICHA ZA TUKIO HILO:
 
IMG 19161
 
 Mkufunzi wa mafunzo ya uongozi kutoka *Taasisi ya Uongozi (Institute of Directors),* Bwana Andulile Mwakalyelye, (kulia ayesimama) akizungumza jambo wakati wa *Semina elekezi* ya uongozi kwa viongozi waandamizi na Viongozi Waandamizi Wakuu wa Shirika la Posta Tanzania katika ukumbi wa NSSF Posta Azikiwe tarehe 29 Mei 2021.
 
 
IMG 19311
 
 
IMG 19261
 Washiriki wa mafunzo ya uongozi wakisikiliza jambo.
 
 
 
IMG 19371
 
IMG 19432
 
 
 
IMG 194611
 
 
IMG 199711
Mkufunzi wa mafunzo ya uongozi kutoka *Taasisi ya Uongozi (Institute of Directors),* Bwana Andulile Mwakalyelye, akizungumza jambo wakati wa *Semina elekezi* ya uongozi kwa viongozi waandamizi na Viongozi Waandamizi Wakuu wa Shirika la Posta Tanzania katika ukumbi wa NSSF Posta Azikiwe tarehe 29 Mei 2021.
 
IMG 202011
 Washiriki wa mafunzo ya uongozi wakiwa kwenye "group discussion"
 
 IMG 204111
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!