POSTA NA UDSM WAKUTANA.

POSTA NA UDSM WAKUTANA.
 
 
IMG 20210603 WA0004
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Daniel Mbodo (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar e's Salaam, Profesa William A.L. Anangisye (kulia) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar e's Salaam Prof. Bernadeta killian.
 
Na Rachel Kitinya
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Daniel Mbodo amekutana na kufanya  mazungumzo ya ushirikiano wa kibiashara na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  
 
Mkutano huo uliofanyika tarehe 2 Juni 2021 kwenye ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar e's Salaam, Profesa William A.L. Anangisye, ulilenga kueleza fursa mbalimbali ambazo chuo hicho kinaweza kuzipata kwa kufanya ushirikiano wa kibiashara baina yake na Shirika la Posta Tanzania, hasa kwenye nyanja ya  usafirishaji, huduma ya duka la mtandao "Posta online shop",  fursa za kupangisha kwenye majengo ya Shirika pamoja na huduma za “Internet cafe”.
 
 
Aidha Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar e's Salaam Prof. Bernadeta killian.
 

 Zifuatazo ni Picha za tukio hilo:
 
IMG 20210603 WA0010
 
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar e's Salaam, Profesa William A.L. Anangisye (kushoto) akizungumza na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Daniel Mbodo (Kulia) wakati wa mazungumzo ya biashara tarehe 2 Juni 2021, kwenye ofisi za Makamu Mkuu wa Chuo huyo.

 
 
IMG 20210603 WA0015
 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar e's Salaam Prof. Bernadeta killian, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo ya kibiashara baina ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shirika la Posta Tanzania.
 
IMG 20210603 WA0009
Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Amos Milinga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Mwandamizi Idara ya Masoko ya Shirika la Posta Tanzania Bwana Kowelo, wakati wa Mkutano wa kibiashara baina ya Shirika la Posta na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
IMG 20210603 WA0014
 
 
 
Imetolewa na Ofisi ya Mawasilian.
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
 

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!