POSTA KUSHIRIKIANA NA GPSA

POSTA KUSHIRIKIANA NA GPSA
 
Na Loema Joseph (TPC)
 
Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Daniel Mbodo leo tarehe 4 Juni, 2021 amekutana na kufanya  mazungumzo ya mashirikiano ya kibiashara na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Prof. Geraldina A. Rasheli, baada ya Shirika la Posta kununua Magari makubwa matano(5) kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na mizigo mbalimbali ikihusisha wadau wenye Huduma ya Ugomboaji na Uondoshaji wa mizigo mikubwa na midogo yaani “Clearing and Forwarding”.  
 
Katika mkutano huo viongozi hao waliweza kujadiliana namna Taasisi hizi mbili za kiserikali zinaweza kushirikiana katika kuhakikisha utoahi wa huduma bora na zenye tija kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
 
Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Prof. Geraldina A. Rasheli, amemshkuru Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo kwa kufika ofisini kwake na amemuahidi ushirikiano katika kutunza mashirikiano haya kwa maendeleo ya Taifa letu.
 
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa GPSA Mwakiselue Mwambange pamoja na Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania ambaye pia ni Msimamizi wa magari hayo Bw. Julius Chifungo. 
 
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano
Shirika la Posta Tanzania.
 
image 648344131
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice D. Mbodo (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Prof. Geraldina A. Rasheli (Mwenye nguo nyekundu), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa GPSA Mwakiselue Mwambange  (Kushoto) pamoja na Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania ambaye pia ni Msimamizi wa magari hayo Bw. Julius Chifungo (Kulia).
 
image 64873271
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice D. Mbodo (Katikati) akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Prof. Geraldina A. Rasheli (Kulia) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa Njombe Bi. Judica Haikase Omari (Kushoto), katika ofisi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), kabla ya mkutano, jijini Dar es Salaam.

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!