PONGEZI

PONGEZI

 

20200615 1643471

Aliyekuwa Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania Bi. Mwanaisha Ali Said.

 

Shirika la Posta Tanzania linatoa pongezi za dhati kwa aliyekuwa Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania (General Manager Business Operations), Bi. Mwanaisha Ali Said kwa kuteuliwa kwake na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kushika nyadhifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar. Uteuzi huo ulifanyaika tarehe 1June 2021.

Bi. Mwanaisha Said aliajiriwa na Shirika la Posta mnamo Machi 2013 kama Meneja Mkaazi wa Shirika la Posta Zanzibar (Resident Manager Posta Zanzibar) hadi mwishoni mwa mwezi Aprili 2018. Ambapo Mei 2018 aliteuliwa kuwa Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara hadi Mei 31 mwaka huu alipoteuliwa tena kushika nyadhifa hii mpya.

Shirika la Posta Tanzania linatambua mchango wa Bi. Mwanaisha Said kama mfanyakazi mchapakazi, mwenye nidhamu na bidii katika usimamizi wa Biashara za Shirika hasa kipindi hiki ambacho Shirika linapitia mabadiliko makubwa ya utoaji wa huduma yanayozingatia ukuaji wa teknolojia.

Tunashuruku kwa mchango wake kwa Shirika, Tunasema ASANTE SANA.

Na Rachel Kitinya:
Ofisi ya Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!