LETENI UBUNIFU WENYE TIJA KWA JAMII - DKT JIM YONAZI.

LETENI UBUNIFU WENYE TIJA KWA JAMII - DKT JIM YONAZI.
 
 
 IMG 24901
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi Akizungumza wakati wa kikao kazi cha Taasisi mbalimbali za kiserikali zinazotoa huduma kwa jamii kwenye makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania Jijini Dar e's Salaam.  Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, huduma za Posta, katika Wizara ya  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bi. Caroline Kanuti.
 
 
Na Rachel Kitinya - TPC
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amefungua kikao kazi cha Taasisi mbalimbali za kiserikali zinazotoa huduma kwa jamii na kuwataka kuwa wabunifu katika kutoa huduma. Ametoa wito huo wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika Makao Makuu ya Shirika la Posta, Jijini Dar  Es Salaam tarehe 9 Juni 2021. 
 
Kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe kutoka Shirika la Posta Tanzania, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mamlaka ya Jiji la Dodoma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),  kililenga kuanzisha vituo vya pamoja vya watoa huduma wa Serikali. 
 
Katika kikao hicho, Dkt. Yonazi alisisitiza taasisi hizo zitoe huduma bunifu, zilizo bora na zenye mifumo rafiki kwa watumiaji ili kurahisisha maisha kwa jamii.
 
Ameongeza kuwa taasisi hizo zibuni mbinu mpya zinazokidhi matakwa ya jamii yanayoendana na hali ya maisha ya sasa.
 
"Sisi tunao wajibu wa kuleta vitu vipya vyenye tija katika kutoa huduma kwa Umma, Na huu mradi  unaoanzishwa utakuja kuwa mradi mkubwa sana. Bila shaka utabadilisha maisha ya jamii yetu pamoja na sisi tuliokaa kikao hiki" Alisisitiza Dkt. Yonazi.
 
Naye Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo ameeleza kuwa, Posta ni kiungo cha kutoa huduma mbalimbali katika taasisi za kiserikali, Hivyo basi ni rahisi zaidi kwa taasisi hizo kutumia fursa hiyo kuhudumia jamii kwa ukaribu zaidi maana Posta inao uzoefu wa kufanya hivyo nchi nzima.
 
Imetolewa na:
 
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania
 
 
PICHA ZA TUKIO HILO:
 
IMG 24712
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo, (kushoto ayesisimama) akizungumza jambo wakati wa wakati wa kikao kazi cha Taasisi mbalimbali za kiserikali zinazotoa huduma kwa jamii kwenye makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania Jijini Dar e's Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Makuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, huduma za Posta, katika Wizara ya  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bi. Caroline Kanuti.
 
IMG 25111
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (katikati mwenye suti ya "Dark blue") akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali za kiserikali zinazotoa huduma kwa jamii kwenye makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania Jijini Dar e's Salaam.
 
 
IMG 24731
 
 
 
 IMG 24861
 
Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za kiserikali zinazotoa huduma kwa jamii wakimsikiliza Naibu Katibu Makuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi wakati wa kikao kazi kwenye Makao Makuu ya Shirika la Posta Jijini Dar e's Salaam,  tarehe 9 Juni 2021.
IMG 24651
 
 IMG 25171
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi, akikagua Magari Makubwa ya Shirika la Posta Tanzania  kwenye makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar e's Salaam.  Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, huduma za Posta, katika Wizara ya  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bi. Caroline Kanuti.
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!