POSTA, COSTECH KUSHIRIKIANA

POSTA, COSTECH KUSHIRIKIANA 
 costech 11
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo (Kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Muhunda Nungu (kushoto) kwenye Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dar e's Salaam, tarehe 9 Jubi 2021.  
 
Na Rachel Kitinya - TPC
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo amekutana na kufanya  mazungumzo ya ushirikiano wa kibiashara na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Muhunda Nungu kwenye Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dar e's Salaam. 
 
 
Kikao hicho kilichofanyika tarehe 9 Juni 2021 kililenga kueleza fursa mbalimbali ambazo Tume hiyo inaweza kuzipata kwa kufanya ushirikiano wa kibiashara baina yake na Shirika la Posta Tanzania, hasa kwenye nyanja ya  usafirishaji, huduma ya duka la mtandao "Posta online shop",  fursa za kupangisha kwenye majengo ya Shirika pamoja na huduma mpya ya Posta kiganjani .  
 
Katika kikao hicho Wakuu hao waliazimia kufanya ushirikiano wa kibiashara na kihuduma utakaonufaisha taasisi zao pamoja na walengwa ambao ni Wananchi. 
 
 
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
 SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
 
 
PICHA ZA TUKIO HILO;
 
costech 31
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Muhunda Nungu (Kushoto) na kulia ni Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Amos Milinga.
 
costech 2
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo (Kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Muhunda Nungu (kushoto) namna ya kujiunga na huduma ya Posta Kiganjani.
 
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!