MAREKANI NA POSTA TANZANIA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA.

MAREKANI NA POSTA TANZANIA KISHIRIKIANA KIBIASHARA.

IMG 25901

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo (kulia) akishika kitabu chenye nembo ya Posta pamoja Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani, Bwana Ken Walsh (kushoto), wa kwanza kulia ni Mtaalamu wa Biashara kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Bi. Mary Msemwa, wapili kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta, Bwana Constantine Kasese, na wa kwanza kushoto ni Meneja Barua wa Shirika la Posta Bwana Jasson Kalile, huku wa pili kushoto ni Meneja Tehama wa Shirika la Posta Bwana David Mtake.

 

 

Na Rachel Kitinya - TPC

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo amekutana na kufanya  mazungumzo na Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani, Bwana Ken Walsh, na kukubaliana kufanya ushirikiano wa kibiashara katika usafirishaji wa vifurushi na barua za wateja kwa njia ya ndege zisizo na rubani "Drones".

Mazunguzo hayo yaliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania,  tarehe 10 Juni 2021 yalilenga kueleza fursa mbalimbali za kibiashara ambazo Marekani na Posta Tanzania zitashirikiana hasa katika nyanja ya usafirishaji wa nyaraka, barua na vifurushi vya wateja kwa maeneo yasiyoweza kufikika kirahisi.

Katika kikao hicho viongozi hao waliazimia kuunda kamati za utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho na kwamba kamati hiyo itakayohusisha pande zote mbili itakuja na mikakati ya utekelezaji wa ushirikiano huo wa kibiashara

Bwana Walsh Aliongozana na Mtaalamu wa Biashara kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Bi. Mary Msemwa.

Imetolewa na:

Ofisi ya Mawasiliano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

 

PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO:

IMG 25681

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo (katikati mwenye suti nyeusi) akisikiliza jambo wakati wa kikao cha makubaliano ya kibiashara baina ya Shirika la Posta na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani nchini.

IMG 25651

Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani, Bwana Ken Walsh (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtaalamu wa Biashara kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Bi. Mary Msemwa wakati wa mazungumzi ya kibiashara baina ya Shirika la Posta na Ubalozi wa Marekani Nchini.

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!