POSTA, OFISI YA TAKWIMU KUSHIRIKIANA

 
POSTA NA OFISI YA TAKWIMU KUSHIRIKIANA.
 
 
 
 
BeautyPlus 20210617171928242 save
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa(kulia)
 
 
Na Rachel Kitinya - TPC
 
Tarehe 17 Juni 2021, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo, alikutana na kufanya mazungumzo na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa na kuona namna Shirika la Posta litakavyoshiriki katika zoezi muhimu la sensa ya watu na makazi linalotarajia kufanyika nchini mwaka 2022.
 
Katika mazungumzo hayo, Mtakwimu Mkuu wa Serikali amempongeza Kaimu Postamasta Mkuu kwa jitihada zinazoendelea kufanyika ndani ya Shirika na amemuhakikishia ushirikiano wa kutosha.
 
Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Jijini Dodoma, yalihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bwana Daniel Andrew.
 
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO:
BeautyPlus 20210617172036361 save
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa(katika), pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bwana Daniel Andrew.
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!