WATANZANIA KUNUFAIKA NA BIASHARA YA MTANDAO KUFIKIA 2025 - DKT. NDUGULILE.

WATANZANIA KUNUFAIKA NA BIASHARA YA MTANDAO KUFIKIA 2025 -  DKT. NDUGULILE.


IMG 20210618 1354161

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza jambo wakati wa mkutano ulioandaliwa na Wizara hiyo, ukihusisha Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo tarehe 16 Juni 2021, Jijini Dodoma.

 

 

Na Rachel Kitinya- TPC

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amesema  Wizara hiyo imejipanga kuwezesha upatikanaji wa intaneti kwa asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2025.


Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati wa mkutano ulioandaliwa na Wizara hiyo, ukihusisha Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimani, Dodoma Juni 16 ,2021 kililenga kuzungumzia mikakati ya Wizara hiyo na Taasisi zake katika Sekta ya Mawasiliano na ukuaji wa uchumi nchini.


Aidha, Dkt. Ndugulile ameeleza kuwa kutokana na janga la Corona biashara mtandao ndio inayoshika kasi kwa sasa, na sisi Tanzania hatupo nyuma sana katika hilo, huku tayari baadhi ya Watanzania hasa vijana wakiwa wadau wakubwa wa biashara hio.


"Sisi kama nchi tunawajibika kutengeneza mazingira wezeshi ili biashara Mitandaoni iweze kukua, lakini tunajukumu la kudigitize shughuli za Serikali, hatuoni furaha mwananchi anapanga foleni bali tunataka apate huduma viganjani, " aliongeza Dkt. Ndugulile.


Aidha,katika maelezo yake Mhe. Dkt. Ndugulile ameeleza nia ya Serikali katika kuboresha huduma za mtandao kwenye sekta ya afya, hata mgonjwa akipiga picha yake ya X-ray isafirishwe mitandaoni ili majibu yapatikane kwa haraka.

Kwa sasa zaidi ya asilimia 90 ya nchi nzima imefikiwa kwa kiwango cha 2G kwa mawasiliano ya kawaida, mawasiliano ya Internet ni asilimia 66, hadi kufikia April, laini za simu zilizosajiliwa zilifika milioni 53 na watanzania milioni 29 wanatumia Internet.

"Tanzania tumepiga hatua sana na Serikali imetumia zaidi ya Bilioni 676 kwenye ujenzi wa Mkongo wa Taifa na tumeunganisha Mikoa yote. Tunataka kuifanya Tanzania kuwa kitovu (hub) ya mkongo miongoni mwa Nchi zinazotuzunguka, na tukimaliza ujenzi Tanzania itakuwa kitovu cha Mawasiliano ukanda huu" Aliongeza Dkt. Ndugulile.


Akimalizia Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inaandaa "Digital economy blue print" ya nchi huku hadi sasa mifumo-mitandao ya uendeshaji wa Serikali kwa zaidi ya asilimia 80 imetengenezwa na vijana wa kitanzania, wakati zamani Serikali ilikuwa ikitumia gharama kubwa kununua mifumo na kugharamia wataalamu wa nje.  Aliongeza kuwa kuwa vijana wengi wamejiajiri katika sekta ya habari, hivyo sekta hiyo ipunguze tozo na gharama za usajili wa vyombo vya habari kwa sababu vijana wengi bado hawana mitaji mikubwa. Serikali inataka kuona sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ina mchango mkubwa kwenye Pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


Kupitia Jukwaa hilo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (MB) alipata nafasi ya kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya maswala yaliyoibuka wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali bungeni. Baadhi ya mambo aliyogusia ni hali ya miradi ya maendeleo nchini, makato ya Kodi na gharama za matumizi ya simu.

"Bajeti yetu imezingatia mambo matatu kwanza hali halisi ya watu wetu, hali ya Kifedha na Masuala ya Kukuza Uchumi tuliangalia kwamba tujibane tupunguze mzigo lakini tukiwa na lengo kule tunataka kwenda" aliongeza kuwa "Hatujaweka "Simcard tax", tunasema mtu ambaye anaweka kuanzia elfu 1000 mpaka 2500 pale alipoweka anatozwa Sh 10 tu, ukiweka laki kwenda juu ni Sh 200 na sio Kila siku alipoweka, ukiweka elfu 50 unatozwa sh 180, elfu 10 hadi 25 ni sh 100 tu, aliyeweka 2500 hadi 5000 anatozwa Sh 21 tu" Alizungumza Mhe. Mwigulu.


Naye Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo akiwasilisha taarifa kuhusu Shirika la Posta na matarajio ya Shirika hilo kwa siku za usoni katika nyanja ya Teknolojia alisema Posta imejipanga kushiriki kuchangia uchumi wa kidijitali kupitia huduma zake.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

 

PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO:

IMG 20210617 WA0053

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (MB) akisisitiza jambo wakati wa mkutano ulioandaliwa na Wizara Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ukihusisha Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, tarehe 16 Juni 2021.

IMG 20210617 WA0089

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (MB), akiwasilisha maelezo ya Wizara hiyo wakati wa mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tarehe 16 Juni 2021, Jijini Dodoma.
 

IMG 20210617 WA0016

Kulia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akijadili jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula (kushoto) wakati wa mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tarehe 16 Juni 2021, Jijini Dodoma.

IMG 20210617 WA0088

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza jambo wakati mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 

IMG 20210617 WA0007

 Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo, akiwasilisha taarifa kuhusu Shirika la Posta na matarajio ya Shirika hilo kwa siku za usoni katika nyanja ya Teknolojia wakati wa Mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tarehe 16 Juni 2021, Jijini Dodoma.

 

IMG 20210617 WA0003

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo, akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari Tanzania na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jijini Dodoma.

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!