"TUNATAKA POSTA YA KIDIJITALI", DKT FAUSTINE NDUGULILE.

"TUNATAKA POSTA YA KIDIJITALI", DKT FAUSTINE NDUGULILE.

IMG 20210701 153211 458

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi na Mpango Mkakati wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tarehe 1 July 2021, Kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

 
Na Mwandishi wetu, Dodoma
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amezindua Tovuti ya Wizara hiyo pamoja na Mpango Mkakati wa Wizara kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2021/22 hadi 2025/26 ambao ni mwongozo wa utendaji kazi na upimaji wa malengo ya Wizara hiyo iliyoyawekea, lengo kuu hasa likiwa kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali na inayoongoza kwenye Biashara mtandao.
 
Hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika tarehe 1/07/2021 kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso(Mb), Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mjumbe  kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Dkt. Ndugulile alieleza kuwa Mpango Mkakati huo umejikita katika nyaraka mbalimbali za kisera na zile za malengo ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa pamoja huku akieleza kuwa Wizara hiyo ina jukumu la kuhakikisha wananchi wanatumia fursa zinazoenda sambamba na maendeleo ya kidijitali kwa kuweka mazingira wezeshi ya mwananchi kupata huduma za kijamii na kiuchumi kwa njia ya mtandao mahali popote alipo.
 
Dkt. Ndugulile alisisitiza kuwa moja kati ya vipaumbele vya Wizara yake ni pamoja na kulifanya Shirika la Posta kuwa la kidijitali. "Ndugu zangu tunataka tuibadilishe Posta, Isiwe tena sehemu ya kutumia barua au kununua stempu pekee, tunataka sasa Posta ya kidijitali, jukumu kubwa litakuwa ni Biashara Mtandao, na Shirika hili kwa sasa litajikita katika Kutoa Huduma ya Pamoja, Kitakuwepo kitu kinaitwa HUDUMA CENTER, ambapo ukienda Posta utaweza kupata Huduma za kifedha na huduma nyingine za Kiserikali".
 
 
"Kwaiyo tunaendelea kufanya mazungumzo na taasisi zingine za Kiserikali, kama NIDA, Vizazi na Vifo (RITA), Maswala ya Kodi za Ardhi, Passport na huduma zingine zote za kijamii zitakuwa zinapatikana mahali pamoja kwenye vituo vya Huduma Center hivyo kwa kupitia Mtandao mpana wa Posta ulioko Nchi nzima, huduma hizi nyingi zilizokuwa zinapatikana sehemu tofauti tofauti, zitaanza kupatikana chini ya Dirisha moja " Alieleza Dkt.Ndugulie. 
 
Akitoa wasilisho la Mpango Mkakati huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula, alieleza kuwa, Mpango Mkakati huu unaoanza tarehe 1July 2021/22 hadi 2025/26 utajikita zaidi katika kuunganisha mifumo ya Wizara zote isomane ili kurahisisha utendaji kazi wa haraka na ufanisi Serikalini, tofauti na sasa ambapo kila Wizara na taasisi zake zina mifumo tofauti tofauti. Kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano,Teknolojia ya Habari, na Huduma za Posta, huku akiomba wafanyabiashara kutumia mtandao wa Posta kujitangaza kibiashara.
 
Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Tovuti ya Wizara ambayo ni www.mawasiliano.go.tz, na Mpango Mkakati, uliambatana na maonesho ya Huduma na Shughuli za Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Shirika la Posta. 
 
 
 
Imetolewa na: 
Ofisi ya Mawasiliano,
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
 
 
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO: 
 
IMG 2872 1
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile (Mb) (mwenye Tai nyekundu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali,  pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake. 
 
 
 
IMG 2871 1
 
 
 
 
 
IMG 20210701 145250 869
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (Kushoto).
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
IMG 2846 1
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Utawala na Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bwana Selemani Mvunye(kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Posta kimataifa, Bwana Elia Madulesi (kushoto)
 
 
IMG 2842 1
 
 
IMG 2828 1
 
 
 
IMG 2818 1
 
 
 
 IMG 2850 1
 
Viongozi mbalimbali wakiwa Kwenye Banda la Shirika la Posta Tanzania wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Wizara Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. 
 
 IMG 2811 1
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (kulia), akizungumza jambo na viongozi mbalimbali, kwenye Banda la Shirika la Posta wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Wizara hiyo. 
 
 
 
IMG 2818 1
 
 Viongozi Waandamizi Wakuu wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 
 
 
IMG 2963 1
 
Viongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Wizara hiyo. 
 
IMG 2942 1
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo(Kushoto) akipokea Mpango Mkakati wa Wizara Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainabu Chaula(kulia). 
 
 
IMG 2951 1
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb)(aliyeinama) akizindua Tovuti Rasmi ya Wizara hiyo.
 
IMG 2959 1
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile (Mb)(mwenye tai nyekundu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake. 
 
 
IMG 20210702 WA0013
 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb)(wa pili kushoto), akizindua Mpango Mkakati wa Wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainabu Chaula na Kulia Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Injinia Kundo Andrea Mathew (Mb).
 
 IMG 20210701 145250 904
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo( wa kwanza kushoto), akiwa Kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Zainabu Chaula (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Injinia Kundo Andrea Mathew(Mb) (kulia)
 
 
IMG 2909 1
 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Posta kimataifa, Bwana Elia Madulesi, akiwa kwenye hafla hiyo.
 
 
IMG 2859 1
 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania Bwana Constantine Kasese (kulia), akiwa kwenye picha ya pamoja na  Kaimu Meneja Mipango, Bi. Oliver Temu. 
 
 
 IMG 2852 1
 
Mtoa huduma wa Shirika la Posta Tanzania, akiwa kwenye Banda la Shirika. 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!