"UCHUMI WA KIDIJITALI NDIYO MKAKATI WA NCHI KWA SASA" DKT NDUGULILE.

"UCHUMI WA KIDIJITALI NDIYO MKAKATI WA NCHI KWA SASA" DKT NDUGULILE.

IMG 20210707 WA0129

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza wakati akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya biashara mtandao baina ya Shirika la Posta Tanzania na Tantrade.

 

Na Mwandishi Wetu,  Dar e's Salaam.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ameeleza kuwa kwa sasa mkakati wa Nchi ni kuelekea kwenye uchumi wa kidigitali ‘Digital Economy’ hivyo Mashirika ya umma yanatakiwa kuwa mstari wa mbele kupokea na kutekeleza mabadiliko haya kwa manufaa ya Taifa na jamii ya watanzania kwa ujumla.

Maneno hayo ameyasema wakati akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kibiashara baina ya Shirika la Posta Tanzania na TANTRADE, yaliyofanyika leo tarehe 7 Julai 2021, kwenye viwanja vya maonesho ya kibiashara ya Sabasaba Jijini Dar e's Salaam.

Dkt Ndugulile amelipongeza Shirika la Posta na TANTRADE kwa maono haya ya kuitumia teknolojia kwa ajili ya kuinufaisha jamii huku ikiwaunganisha Wafanyabiashara eneo moja na kuwatambulisha katika soko la ndani na nje ya Nchi kupitia Duka hilo la Mtandao.

"Duka hili litamuwezesha mteja kuuza,
kutangaza na kununua bidhaa tofauti tofauti ndani na nje ya nchi kupitia mtandao. Miamala ndani ya duka hili itafanyika mtandaoni, baada ya kujisajili kupitia tovuti rasmi ya duka hili ambayo ni www.PostaShoptz.post" Alizungumza Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile alilitaka Shirika la Posta kuliunganisha duka hili la mtandao na maduka mengine ya mtandano ya Posta zingine duniani ili kuongeza soko la bidhaa za Tanzania nje ya Nchi.

Kwa upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), amempongeza Waziri wa Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile na Katibu Mkuu wake, Dkt Zainab Chaula, kwa kazi kubwa wanayoifanya ndani ya Wizara hiyo, huku akisisitiza kuwa, Katika mabadiliko ya kihuduma yanayofanywa ndani ya Shirika la Posta, yasiondoe huduma nzuri za zamani za Shirika hilo kama utumaji wa barua kwenye sanduku la barua ili kuifanya Posta ibaki na uhalisia wake.

Dkt. Mkumbo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Bwana Macrice Daniel kwa kazi kubwa anayo ifanya ya mageuzi ya huduma za kiteknolojia ndani ya Shirika.

Nae Kaimu Postamasta Mkuu, Bwana Macrice Mbodo alieleza mabadiliko mbalimbali ya kihuduma yanayofanywa ndani ya Shirika la Posta hasa kwenye eneo Kidijitali na matumizi ya Duka Mtandao la Posta na namna ya kujiunga na duka hilo.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

 

IMG 20210707 WA0134

Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Balozi Mteule Edwin Rutegaruka(kushoto), akisaini hati ya makubaliano ya kibiashara na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (kulia), wakati wa hafla ya utiaji saini huo. 

 

IMG 20210707 WA0133

 Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Balozi Mteule Edwin Rutegaruka (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (kulia) wakati wa hafla hiyo.

 

IMG 20210707 182417 206

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.

IMG 20210707 182417 207

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 

IMG 20210707 WA0116

 Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo, akielezea huduma ya Duka Mtandao "Posta Online Shop " wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya kibiashara ya duka mtandao baina ya Shirika la Posta na TANTRADE. 

 

IMG 20210707 WA0107

 Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Balozi Mteule Edwin Rutegaruka, akizungumza wakati wa Hafla hiyo.

 

IMG 20210707 WA0101

 Wakuu wa Taasisi Mbalimbali za Kiserikali waliohudhuria katika hafla ya utiaji saini wa Makubaliano ya Biashara Mtandao baina ya Shirika la Posta na TANTRADE.

 

IMG 20210707 WA0125 

Viongozi, Wakuu wa Taasisi, Wafanyabiashara na Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania na TANTRADE wakimsikiliza Waziri wa Viwandana Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

 

IMG 20210707 WA0120

 Mtumbuizaji, Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla hiyo.

IMG 20210707 WA0109

 Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (kulia mwenye suti ya Bluu), akisikiliza jambo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya biashara mtandao baina ya Shirika la Posta Tanzania na TANTRADE. 

 

IMG 20210707 WA0136

Wakuu wa Taasisi mbalimbali wakiwa Kwenye picha ya pamoja na Mawaziri. 

IMG 20210707 WA0140

 Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa kwenye picha ya Pamoja na Mawaziri.

 

IMG 20210707 WA0094

Watumbuizaji wa hafla hiyo. 

 IMG 3155 1

Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania , Bwana Aron Ayyo (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Mwandamizi wa Shirika hilo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya biashara mtandao baina ya Shirika la Posta na TANTRADE. 

 

IMG 3193 1

Mameneja Mbalimbali wa Shirika la Posta wakiwa kwenye hafla ya Utiaji saini wa makubaliano ya biashara mtandao baina ya Shirika la Posta na TANTRADE.

IMG 20210707 WA0168

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo.

 

IMG 20210707 WA0166

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa mbele ya Banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Sabasaba.

 

IMG 20210705 WA0003

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa ndani ya Banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Sabasaba.  

 

20210708 122526

 Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa ndani ya Banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Sabasaba.

 

 

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!