INJINIA KUNDO AKAGUA MIRADI YA MAWASILIANO, MTWARA.

INJINIA KUNDO AKAGUA MIRADI YA MAWASILIANO, MTWARA. 
IMG 20210715 154817 602
 
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia  ya Habari, Mhe. Injinia Kundo Andrea Mathew (Mb) (Katikati mwenye Suti ya Bluu) akiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jenerali Marco E. Gaguti wakati alipotembelea Mkoa huo, ili kukagua miradi Mbalimbali inayotekelezwa Chini ya Wizara yake.
 
 
 
Na Mwandishi Wetu, Mtwara 
 
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Injinia Kundo Andrea Mathew(Mb.) amefanya ziara ya kikazi Mkoani Mtwara na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na iliyokamilika ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF). 
 
Ziara hiyo iliyofanyika tarehe 11 Julai 2021, pamoja na mambo mengine, ililenga kuhakiki maeneo yenye changamoto za Mawasiliano, kukagua hali ya mwingiliano wa mawasiliano mipakani, kuhamasisha Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi, kukagua Mkongo wa Taifa na kukagua utendaji wa ofisi za Posta na TTCL Mkoani humo.
 
Akiwa kwenye ziara hiyo, Injinia Kundo, alipokea taarifa ya utendaji wa Shirika la Posta Tanzania na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo Mkoani humo, kutoka kwa Kaimu Meneja wa Posta Mtwara, Bwana Gerald John Kessy. 
 
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano 
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
IMG 20210715 154817 623
 
Kaimu Meneja wa Posta Mtwara, Bwana Gerald John Kessy akizungumza  wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Injinia Kundo Andrea Mathew (Mb), kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa , Wabunge wa Mkoa huo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.
 
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!