SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA BIMA ZANZIBAR.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo(kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), Bwana Arafat Haji(kushoto).
Shirika la Posta Tanzania katika kuendelea kuboresha huduma zake Tanzania Bara na Visiwani, Leo tarehe 15 Julai Mjini Zanzibar limetiliana saini ya mashirikiano ya kiashara na Shirika la Bima la Zanzibar.
Shirika la Posta limeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuanzishwa kwa Duka la Mtandao, Huduma Pamoja( pamoja Center) pamoja na huduma ya Posta Kiganjani sasa imehamia Visiwani Zanzibar kwa kuingia Mkataba wa mashirikiano ya Kibiashara na Shirika la Bima la Zanzibar.
Hafla ya utiaji wa saini umefanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Bima la Zanzibar Katika Visiwa vya Zanzibar Leo tarehe 15Julai,2021. Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo alikuwa Dk. Juma Malik Akili Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Dk. Juma Malik Akili ametoa pongezi za dhati kwa mashirika yote mawaili Shirika la Posta Tanzania pamoja na Shirika la Bima Zanzibar kwa kuweza kuungana katika kufanya kazi. Dk. Juma Malik amendelea kwa kuutaka Ushirikiano huwo ukawe Ushirikiano wenye faida kwa pande zote mbili upande wa Posta pamoja na Upande za Shirika la Bima la Zanzibar.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar, Bwana Arafat Haji, amesema kuwa Shirika la Bima la Zanzibar lipo tayari kufanya na Shirika la Posta kwani Mashirika yote ni ya Serikali na ni fursa kwa Shirika la Bima la Zanzibar kueneza huduma kwa Upande wa Tanzania Bara na Visiwani.
Aidha Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel ameeleza kuwa Shirika la Posta kwa sasa linaendele kuboresha huduma zake lengo ni kumfanya Mwananchi amepata huduma bora kutoka katika Shirika hilo.
Mkataba huo wa mashirikiano ya kibiashara utawawezesha Wananchi kupata Bima kupitia katika Shirika lao la Posta Tanzania.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano,
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar, Bwana Arafat Haji (kushoto).
Wakisaini mikataba wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar, Bwana Arafat Haji akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Bi. Mwanaisha Ali Said, (kushoto) akiwa Kwenye picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (kulia).