POSTA NA TANTRADE WATOA MAFUNZO YA MIFUMO YA BIASHARA MTANDAONI ZANZIBAR.

POSTA NA TANTRADE WATOA MAFUNZO YA MIFUMO YA BIASHARA MTANDAONI ZANZIBAR.
 
 IMG 20210723 WA0001
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Daniel Mbodo akizungumza katika mafunzo hayo,  jijini Zanzibar.
 
Na Mwandishi wetu Zanzibar,
 
Tarehe 22 Julai , 2021, Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na TanTrade wametoa Mafunzo ya Mifumo ya Biashara mtandaoni kwa Wafanya Biashara pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kibiashara Visiwani Zanzibar.
 
 Mifumo iliyofundishwa ni Mfumo wa Duka mtandao (Shirika la Posta), Mfumo wa Information Portal Market Access Map pamoja na Mfumo wa E-malalamiko. (TanTrade)
 
Mgeni Rasmi katika tukio Hilo alikuwa Dkt. Islam Salum Seif, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Dkt. Islam ametoa pongezi kwa Shirika la Posta pamoja na TanTrade kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatakwenda kuwasaidia maafisa wote wanao simamia biashara pamoja na Wafanya Biashara wa Zanzibar. 
 
Aidha,Katibu Mkuu huyo amesema mifumo hiyo ya biashara itawasaidia wafanya biashara wa Zanzibar kutangaza biashara zao hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa Ugonjwa wa Corona." Katika kipindi hiki ambapo dunia imekumbwa na ugonjwa wa Covid-19 wafanya biashara wameendelea kufanya biashara kupitia maduka ya mtandaoni, na wanafanya biashara bila ya kukutana ana kwa ana, hivyo mifumo hii itakwenda kuwasaidia wafanya biashara wa Zanzibar." Alisema Dkt Islam.
 
Naye Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo ameeleza namna ambavyo Shirika la Posta limejipanga katika kutoa huduma kwa Wananchi wa Zanzibar pamoja na Tanzania bara. 
"Shirika la Posta tumefanya maboresho makubwa katika kutoa huduma sasa tumetoa fursa kwa wafanya biashara kutangaza biashara zao kupitia mfumo wa duka mtandao" Alisema Bwana Mbodo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Balozi Mteule Edwin Rutageruka amesema Mifumo hiyo inaenda kutekeleza azma ya Serikali ya kukuza Uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
" Mifumo hii itaenda kutekeleza azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza Uchumi wetu" Alisema Balozi Edwin Rutageruka.
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILI
 
IMG 20210723 WA0000
 
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Islam Salum Seif (katikati),  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Balozi Mteule Edwin Rutageruka (kulia kwake),  Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo na kushoto kwa Dkt Seif ni Makamu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa Khamis akifuatiwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara Zanzibar Ndugu Hamadi Hamadi.
 
 
 IMG 20210723 WA0002
 
 Meneja Biashara Mtandao wa Shirika la Posta Tanzania, Bi Amina Salum Mohamed akielezea namna ya kujisajili katika Duka Mtandao pamoja na namna ya kutumia mfumo wa Duka mtandao katika Mafunzo ya Mifumo ya Biashara yaliyo fanyika Visiwani Zanzibar Leo tarehe 22 Julai,2021.
 
 IMG 20210723 WA0003
 
Meneja Mkaazi wa Shirika la Posta Jijini Zanzibar, Bw. Khamis Ahmad Swedi akiwasilisha changamoto kubwa ya wafanya Biashara wa Zanzibar kwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Dkt Islam Salum Seif Leo wakati wa mafunzo ya Duka mtandao.
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!