POSTA NDANI YA MAONESHO YA VYUO VIKUU.

POSTA NDANI YA MAONESHO YA VYUO VIKUU.
 
IMG 20210728 182424 087
 

Wa kwanza kushoto ni Afisa Mifumo Mwandamizi wa Shirika la Posta, Mhandisi Fifi kulwa na Afisa Masoko Mwandamizi Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bi. Happines Iteba(wa pili kushoto) wakizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, Mhandisi Nseya L. Kipilyango(katikati) wakati alipotembelea Banda hilo kwenye maonesho ya vyuo vikuu ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar e's Salaam. Wa kwanza kulia ni Bwana Evord Mwauzi(Afisa Masoko Mwandamizi Mkuu) na wa pili Kulia ni Bwana Innocent Fabian, Mkuu wa Kitengo cha Masoko kwenye Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali.

 
 
Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam
 
Shirika la Posta Tanzania linashiriki maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja, Jijini Dar e's Salaam. Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 26 Julai 2021 na kutarajiwa kumalizika tarehe 31 Julai 2021 yanahusisha vyuo vikuu mbalimbali nchini, nje ya Nchi, wadau wa elimu, wadhamini wa vyuo vya elimu ya juu na Taasisi mbalimbali za elimu ndani na nje ya nchi. 
 
Posta ikiwa kama mdau wa elimu Nchini inawakaribisha wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu kufika kwenye Banda la Shirika hilo kuchukua na kurudisha fomu za maombi ya mikopo ndani ya viwanja hivyo.
 
Aidha tunakaribisha Taasisi mbalimbali za elimu, Wanafunzi na Wananchi kwa ujumla kufika katika Banda la Shirika la Posta kupata huduma ya masanduku ya barua kupitia simu ya mkononi, (Posta kiganjani) ambapo namba ya simu ya mteja ndio itasajiliwa kama Sanduku lake la barua. 
 
Imeandaliwa na:
Ofisi ya Mawasiliano 
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA 
 
 
 
IMG 20210728 182424 141
 
Afisa Posta, Bwana Christopher Mhando akizungumza na mteja.
 
 
IMG 20210728 182424 098
 
 

Afisa Masoko Mwandamizi Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bi. Happines Iteba(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, Mhandisi Nseya L. Kipilyango(katikati) wakati alipotembelea Banda hilo ndani ya maonesho ya Vyuo Vikuu, kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar e's Salaam. Wa kwanza kulia ni Bwana Evord Mwauzi(Afisa Masoko Mwandamizi Mkuu) na wa pili Kulia ni Bwana Innocent Fabian, Mkuu wa Kitengo cha Masoko kwenye Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali.

 
IMG 20210728 182424 138
 
Afisa Masoko Mwandamizi Mkuu Bwana Evord Mwauzi(kushoto) akiwa na mteja.
 
 
 IMG 20210728 182424 145
 
 

Afisa Mifumo Mwandamizi wa Shirika la Posta, Mhandisi Fifi kulwa akiwa kwenye Banda la Shirika.

 

IMG 20210728 182424 133

Wanafunzi mbalimbali wa Elimu ya Juu wakipokea maelezo ya kutuma fomu za maombi ya mikopo ndani ya Viwanja vya Mnazi mmoja kwenye maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea wiki hii.

 

IMG 20210728 182424 113

Wanafunzi mbalimbali wa Elimu ya Juu wakiwa kwenye Banda la Shirika la Posta.

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!