POSTA IKO VIWANJA VYA MNAZI MMOJA.

POSTA IKO VIWANJA VYA MNAZI MMOJA.

IMG 20210729 WA0066

Afisa Mifumo Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania,  Mhandisi Fifi Kulwa akitoa maelezo kwa mwanafunzi wa Elimu ya juu aliyefika kwenye banda hilo.

 

 

Na Mwandishi Wetu, Dar e's Salaam. 

Shirika la Posta linawakaribisha Wadau wa elimu, Wanafunzi wa Elimu ya Juu na wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu kufika kwenye Banda la Shirika hilo, lililoko kwenye maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar e's Salaam.

Shirika linawakaribisha Wanafunzi wa Elimu ya Juu, kuchukua na kurudisha fomu za maombi ya mikopo kupitia Banda la Shirika la Posta ndani ya viwanja hivyo. Aidha tunawakaribisha wadau mbalimbali kujiunga na huduma za Posta za Kidijitali kama vile "Posta Kiganjani", duka la Posta Mtandao "Posta Online Shop" na kupata maelezo ya huduma nyingine mbalimbali za kutuma vifurushi, Barua, nyaraka na mizigo mbalimbali mikubwa.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 31 Julai 2021.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano,
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

 

IMG 20210729 WA0065

Wateja mbalimbali wakiwa Kwenye Banda la Shirika la Posta kwenye maonesho hayo.

 

IMG 20210729 WA0063

Afisa Posta Christopher Mhando akihudumia mteja. 

 

IMG 20210729 WA0067

 

BeautyPlus 20210730125432750 save

Afisa Posta akihudumia mteja

Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!