TANZANIA YASHIRIKI KIKAO CHA PILI CHA MKUTANO MKUU WA 27 WA UMOJA WA POSTA DUNIANI

TANZANIA YASHIRIKI KIKAO CHA PILI CHA MKUTANO MKUU WA 27 WA UMOJA WA POSTA DUNIANI.
 
BEAUTY PLUS save
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainabu Chaula (kulia) akisikiliza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani.
 
 
 
 Abidjan. Ivory Coast  Tarehe 24 Agosti, 2021
 
Katibu Mkuu ,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bwana Amour Hamil Bakar  wamehudhuria kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani unaoendelea jijini Abidjan,Ivory Coast.
 
Mkutano huu , pamoja na mambo mengine Utafanya Uchaguzi wa viongozi wakuu wa Umoja huo ambao ni Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 25 Agosti,2021 .
Wanaowania nafasi za Mkurugenzi Mkuu ni Bw. Pascal Clivaz kutoka nchi ya Uswiss, Bwana Jack Hamande kutoka Ubelgiji na Bwana Masahiko Metoki kutoka Japan.
 
Wanaowania nafasi ya Unaibu Mkurugenzi Mkuu ni Bi. Marcela Maron wa Ajentina , Bwana Younouss Djibrine,Kameruni ,Bwana Marjan Osvald, wa Slovania na Vladyslav Dubenko wa Ukraine.
 
Mkutano Mkuu huo pia utachagua wajumbe wa mabaraza ya Umoja huo, yaani Baraza la Utawala na Baraza la Uendeshaji katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 26 Agosti,2021.
 
 
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
 
BEAUTY PLUS 2save
 
Katibu Mkuu ,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Zainabu Chaula(kulia), akikabidhi zawadi ya Tanzania kwa mwakilishi kutoka Nchi ya Oman Bwana Ahmed Al-Aamri(kushoto) baada ya mazungumzo ya kuungwa mkono kwenye uchaguzi wa Mabaraza ya Utawala na Uendeshaji ya Umoja wa Posta Duniani ambayo Tanzania inagombea.
Anayesimama katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu wa  Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo.
 
 
 BeautyPlus 20210825184239899 save
 
 
Katibu Mkuu ,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula(kulia) akifanya mazungumzo ya kuomba uungwaji mkono wa Tanzania kwenye uchaguzi wa Mabaraza ya Utawala na Uendeshaji ya Umoja wa Posta Duniani ambayo Tanzania inagombea kutoka kwa mwakilishi wa Nchi ya Marekani, Bwana Joseph Murphy (katikati) wakati wa Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani.
Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa  Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo.
 
 
BeautyPlus 20210825190120801 save
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa  Shirika la Posta Tanzania, Bwana Macrice Mbodo (kulia) akizungumza na Bwana Ahmed Al Aamri kutoka Oman kuhusiana na ushirikiano wa kibiashara baina y Posta Tanzania na Posta ya Oman, mazungumzo hayo yamefanyika jijini Abidjan,Ivory Coast.
 
 
IMG 20210826 081605
 
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Mhandisi Clarence Ichwekeleza(Kulia)akizungumza na Mjumbe kutoka Nchi ya Ukrain Bi. Julia Pavlenko(kushoto) alipokuwa akiomba uunvwaji mkono wa mgombea wa UKrain, kwenye nafasi ya Unaibu Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani Bwana Vladyslav Dubenko(katikati).
 
 IMG 20210826 081622
 
 Kaimu Postamasta Mkuu Bwana Macrice Mbodo(kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika ,Bi. Jessica Uwera(katikati) pamoja na Mgombea kiti cha Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani Bwana Jack Hamande wa Ubelgiji(kulia) wakati wa vikao vinavyoendelea vya Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani jijini Abidjan,Ivory Coast.
 
 
 IMG 20210826 081646
 
Kaimu Postamasta Mkuu Bwana Macrice Mbodo(kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika ,Bwana Chief Moyo wakati wa vikao vinavyoendelea vya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani jijini Abidjan,Ivory Coast.
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!