UMOJA WA POSTA DUNIANI WAPATA MKURUGENZI MKUU MPYA.

 
 
UMOJA WA POSTA DUNIANI  WAPATA MKURUGENZI MKUU MPYA.
 
 IMG 20210826 WA0006
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) Ndugu, Masahiko Metoki (wa pili kushoto). Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Posta Zimbabwe (ZIMPOST) Bwana Isaac Muchokomori, anayefuatia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza,  akifuatiwa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Daniel Mbodo(wa kwanza kulia). 
 
 
 
 
Abidjan, Ivory Coast, Tarehe 25 Agosti,2021
 
Mkutano Mkuu wa Umoja 27 wa  Umoja wa Posta Duniani leo tarehe 25 Agosti Umemchagua raia wa Japan, Bwana  Masahiko  Metoki kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Umoja huo kwa kipindi cha miaka minne 2022-2025 kufuatia uchaguzi uliofanywa na wajumbe wa Mkutano Mkuu huo.
 
Bwana Metoki amewashinda wagombea wezake kwa kupata kura  102 akifuatiwa na mgombea mwingine Bwana Pascal Clivaz kutoka nchi ya Uswis aliyepata kura 40 na Bwana Jack Hamande kutokea Ubelgiji aliyepata kura 14.   
 
Mkutano huo pia umemchagua Bwana  Marjan  Osvald kutoka Slovania kwa kura 86 dhidi ya wagombea wenzake Bwana Younouss Djibrine kutoka Kameruni aliyepata kura 47 na Bi Marcela Maron wa Ajentina aliyepata kura 21.
 
Tanzania imeongozwa na Dkt.Zainab Chaula katika Mkutano huo ambao unatarajia pia kuchagua wajumbe wa mabaraza ya Umoja wa Posta Duniani (Baraza la Utawala na Baraza la Uendeshaji) tarehe 26 Agosti,2021. Tanzania inagombea mabaraza yote mawili katika uchaguzi huo.
 
Imetolewa na:
Kitengwo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania.
 
IMG 20210826 WA0005
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Umoja wa Posta Duniani,  Ndugu Masahiko Metoki (kulia).
 
 
FB IMG 1629967199312
 
 
 
BeautyPlus 20210826123519483 save
 
 
 
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!