POSTA KUENDELEA KUWAHUDUMIA WAOMBAJI MIKOPO ELIMU YA JUU.  

POSTA KUENDELEA KUWAHUDUMIA WAOMBAJI MIKOPO ELIMU YA JUU.
 
 
IMG 20210902 WA0131
 
Mwakilishi wa Kaimu Postamasta Mkuu na Meneja wa EMS, Bwana Mbarouk Sasilo akizungumza wakati wa kikao chake na Bodi ya Mikopo ya Elimu juu (HESLB).
 
 
 
Na Mwandishi Wetu, Dar e's Salaam. 
 
Mwakilishi wa Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Mbarouk Sasilo ameelezea namna ambavyo Shirika la Posta Tanzania lilivyowahudumia wanafunzi waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kupitia ofisi za Shirika hilo zilizopo nchi nzima.
 
Hii ni kufuatia mkutano wa Bodi ya mikopo na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 01 Septemba, 2021 jijini Dar es Salaam, ukilenga kuelezea mafanikio na changamoto zilizojitokeza kufuatia kumalizika kwa muda wa kufanya maombi ya mikopo ya elimu ya juu uliyoanza mwanzoni mwa Agosti, 2021.
 
Bw. Sasilo alieleza kuwa, hadi kufikia jana, Agosti 31, 2021 TPC ilikua imepokea na kuchakata fomu za wanafunzi wapatao 56,140 na kuziwasilisha ofisi za HESLB na nyingine 2,200 zikiwa bado njiani kufikishwa HESLB.
 
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru ameweka bayana kuwa Bodi hiyo inaendelea kupokea marekebisho ya fomu chache ambazo waombaji wamekosea ili kuhakikisha kuwa  kila anayehitaji mikopo hiyo anapata fursa ya kuwasilisha maombi yake pasipo mapungufu. 
 
Aidha, Bw. Badru ameongeza kuwa wanafunzi waliopo Kambi za Majeshi ya Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria ambao hawakufanikiwa kuwasilisha maombi yao watapata nafasi ya kufanya hivyo kuanzia tarehe 20 hadi 30 mwezi Septemba 2021.
 
Mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa HESLB jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mwakilishi kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Beatrice Mboya, maafisa kutoka Shirika la Posta Tanzania na maafisa kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
 
Imetolewa na;
Ofisi ya Mawasiliano
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA. 
 
 
PICHA ZA TUKIO HILO: 
 
 IMG 20210902 WA0129
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam, ambapo wametangaza kuongeza muda wa siku 15 kwa waombaji mikopo kuanzia Septemba 1 hadi 15 2021.
 
 
 
IMG 20210902 WA0130
 
Mwakilishi wa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mbarouk Issa akizungumzia namna ambavyo Shirika limehudumia wanafunzi kwa kipindi cha maombi ya Mkopo wa elimu ya juu, wakati wa Mkutano wa HESLB na waandishi wa habari, tarehe 1 Septemba, 2021, jijini Dar es Salaam.
 
 
 IMG 20210902 WA0124
Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Beatrice Mboya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano uliofanyika katika ofsi za HESLB, jijini Dar es Salaam.
 
 
 IMG 20210902 WA0127
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru (katikati) akiwa na Mwakilishi wa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mbarouk Issa Sasilo (kulia) na Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Beatrice Mboya, wakati wa mkutano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi  wa elimu ya juu (HESLB) na waandishi wa habari,terehe 1/9/2021, katika ofisi za bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 
 
 IMG 20210902 WA0125
 
 Maafisa kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea katika ofisi za HESLB, jijini Dar es Salaam, tarehe 1/9/2021.
 
 
 
 
IMG 20210902 WA0132
Maafisa masoko kutoka Shirika la Posta Tanzania wakifuatilia mkutano uliokuwa unafanyika katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam, ambapo wametangaza kuongeza muda wa siku 15 kwa waombaji mikopo kuanzia Septemba 1 hadi 15 2021.
 
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!