MBODO: JIANDAENI KIKAMILIFU MNAPOSHIRIKI VIKAO.

MBODO: JIANDAENI KIKAMILIFU MNAPOSHIRIKI VIKAO.
 
>Makamu wa Rais, kuwa mgeni Rasmi Siku ya Posta Duniani.
 
>Dola za Kimarekani milioni 21.5 kuwezesha mradi wa Huduma Pamoja.
 
 
Moro
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta, kilicholenga kujadili maslahi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo, katika ukumbi wa Edema, mjini Morogoro.
 
 
 
Na mwandishi wetu, Morogoro.
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Daniel Mbodo amewataka wajumbe wa Baraza la majadiliano la Shirika hilo kufanya majadiliano kwa weledi na kujiandaa kikamilifu pindi wanaposhiriki majadiliano hayo ili majadiliano hayo yawe na tija kwa Shirika lenyewe na kwa wafanyakazi.
 
‘’Iweni na nia njema mnapoelekea kwenye kikao cha majadiliano ili kikao hiki kiwe na tija kwa pande zote mbili, mitazamo yenu ielekezeni kwenye agenda liyoko mbele yenu na siyo nje ya hapo alisisitiza Bwana Mbodo"
 
Haya aliyasema leo tarehe 8 mwezi Septemba,   2021 wakati alipokuwa akifungua rasmi kikao cha Baraza la majadiliano kinachofanyika katika ukumbi wa Edema, mjini Morogoro kinachohudhuriwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wawakilishi wa menejimenti ya Shirika hilo.
 
Aidha, Kaimu Postamasta Mkuu alitumia nafasi hiyo kutoa taarifa ya maendeleo ya Shirika kwa ujumla na mikakati ya Shirika ya kuongeza mapato kwa ajili ya ustawi wa Shirika lenyewe, wafanyakazi na taifa kwa ujumla. 
 
Pia aliwafahamisha wajumbe wa Baraza hilo kuwa Serikali Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango nchini imelipatia Shirika la Posta kiasi cha shilingi Bilioni 3.9 kati ya Bilioni 7.9  zilizotumiwa na Shirika hilo kulipa  mafao ya wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la  Afrika mashariki lililovunjika mwaka 1977.
 
Ameeleza kuwa tayari Shirika limeshapeleka mapendekezo kwa Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari namna ambavyo litazitumia fedha hizo kuboresha na kuongeza vitendea kazi ikiwemo magari, kompyuta na kuimarisha mifumo ya kuteknolojia ili kulifanya Shirika kuwa la kidigitali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuwahudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja.
 
‘’Serikali kupitia Wizara ya Fedha imelipatia Shirika la Posta kiasi cha Shilingi bilioni 3.9 na tayari tumewasilisha mapendekezo Wizarani ya namna ambavyo fedha hizo tutakwenda kuzitumia lakini sehemu kubwa ya matumizi ya fedha hizo ikiwa ni kuboresha vitendea kazi ikiwemo magari, kompyuta ili wafanyakazi wa Posta waweze kufanya kazi katika mazingiora rafiki’’. Alisema Mbodo.
 
Vilevile, Mbodo alilielezea Baraza hilo namna ambavyo Tanzania kupitia Shirika la Posta limefanikiwa kuiwakilisha vyema nchi ya Tanzania kwa kufanikiwa kushinda nafasi mbili muhimu kwenye Umoja wa Posta Duniani wakati wa Mkutano wa 27 wa Umoja huo uliofanyika nchini Ivory Coast mwezi Agosti, 2021. 
 
Katika mkutano huo Tanzania imeshinda nafasi ya kuwa mjumbe wa Baraza la Utawala na Baraza la Uendeshaji la Umoja wa Posta Duniani. Pia Tanzania imefanikiwa kuwa mmoja wa wenyeviti wa kamati muhimu inayohusiana na biashara mtandao katika mkutano huo.
 
Kaimu Postamasta Mkuu alieleza mkakati wa Serikali kwa Shirika la Posta kupitia mradi wa Vituo vya Huduma Pamoja ambapo mpaka sasa zimetengwa Dola za Kimarekani milioni  21.5 kuwezesha mradi huo ambao utawawezesha wananchi kupata huduma zote za Serikali kwenye eneo moja kwa wepesi na uharaka zaidi.
 
Sambamba na hili, Mbodo alipata nafasi ya kueleza mkakati wa kuiadhimisha siku ya Posta Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Oktoba. Amesema madhimisho ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee, ambapo kwa mwaka huu mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango. Pia siku hiyo itaambatana na wiki ya Posta.
 
Katika hatua nyingine, Kaimu Postamasta Mkuu ameeleza mwelekeo wa Shirika katika kuifanya Posta ya kidigitali ambapo Shirika litajikita zaidi kwenye Biashara Mtandao [E-Commerce] na kuimarisha huduma za usafirishaji kwa kuanzisaha Kitengo cha usafirishaji kinachojitegemea ili kutafuta biashara na masoko na kuongeza mapato kwa Shirika.
 
Pia, alieleza namna ambavyo Shirika linaendelea kukuza mahusiano ya kibiashara na Mashirika na Taasisi mbalimbali nchini ambapo mpaka sasa Shirika limejenga mahusiano mazuri ya kibiashara na Shirika la Ndege nchini [ATCL], NMB, Benki ya mkombozi, CRDB, Mamalaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), NBC na nyingine nyingi, lengo likiwa ni kuwafikia wananchi kwa wakati na kwa urahisi. 
 
Naye Mwenyekiti wa Baraza hilo Bwana Omari M. Dibibi amempongeza Kaimu Postamasta Mkuu kwa utendaji wake na amemshukuru kwa kukubali kufungua kikao hicho na kumuahidi kuendesha mkutano huo kwa weledi ili kuleta matokea chanya kwa Shirika kama ilivyokusudiwa. 
 
Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Wafanyakazi Junus Ndaro alipongeza juhudi zilizofanyika na mikakati mizuri inayoonekana ya kuboresha utendaji wa Shirika ikiwa ni sehemu ya kuliboresha Shirika la Posta nchini kwa maslahi mapana ya taifa letu.
 
 
Imetolewa na:
Kitengo cha  Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
8 Septemba, 2021.
 
 
 IMG 20210909 WA0005
 
Mwenyekiti wa Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta Tanzania, Omari M. Dibibi akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo, mjini Morogoro.
 
 
IMG 20210909 WA0006
 
Msemaji Mkuu wa Wafanyakazi wa Shirika la Posta nchini Junus Ndaro akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao cha Baraza la Majadiliano, Morogoro
 
IMG 20210909 WA0011
 
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Majadiliano wa Shirika la Posta, mara baada ya kufungua rasmi Baraza hilo, katika ukumbi wa Edema, Morogoro
IMG 20210909 WA0012
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta, kilicholenga kujadili maslahi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo, katika ukumbi wa Edema, mjini Morogoro
 
IMG 20210909 WA0008
 
Wajumbe wa Baraza la Majadiliano wa Shirika la Posta Tanzania wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea wa Baraza hilo, katika ukumbi wa Edema, mjini Morogoro
 
 
 
IMG 20210909 WA0009
 
Wajumbe wa Baraza la Majadiliano wa Shirika la Posta Tanzania wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea wa Baraza hilo, katika ukumbi wa Edema, mjini Morogoro
 
 
IMG 20210909 WA0010
 
 
Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta nchini Constantine Kasese (kushoto) akiteta jambo na Meneja Rasilimali watu wa Shirika la Posta Miriam Mmbaga (kulia), wakati wa mkutano wa Baraza la Majadiliano la Shirika la Posta nchini uliofanyika mjini Morogoro
 
 
IMG 20210909 WA0013
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo akiimba wimbo wa Wafanyakazi na wajumbe wa Baraza la Majadiliano wa Shirika la Posta, mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza hilo, katika ukumbi wa Edema, Morogoro leo.
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!