MKURUGENZI MKUU WA POSTA IVORY COAST ATEMBELEA POSTA TANZANIA.

MKURUGENZI MKUU WA POSTA IVORY COAST ATEMBELEA POSTA TANZANIA.

Kasese  
Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao akizungumza wakati wa kikao chake na Menejimenti ya Shirika la Posta, katika Makao Makuu ya Shirika , jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese.
 
 
 
 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao, ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Jijini Dar e's Salaam na kujionea namna Shirika hilo linavyofanya kazi zake hasa katika kipindi hiki cha ukuaji wa Teknolojia.

 

Ziara hiyo iliyofanyika leo tarehe 13 Septemba, ililenga kukuza ushirikiano baina ya Posta za Nchi hizi mbili pamoja na kuangalia fursa za kibiashara zitakazowezesha kukuza pato la Mashirika haya.

 

Katika ziara yake Ndugu Isaac,  alipokelewa na  Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese ambae alieleza hatua mbalimbali zilizofikiwa na Shirika la Posta Tanzania katika utoaji huduma kiteknolojia. 

 

Aidha Ndugu Isaac  alipata nafasi ya kuongea na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania huku akiwataka kuongeza bidii na kuwa wanyumbufu katika kutoa huduma kwa niaba ya Serikali Ili kuwafikia wananchi.

 

Alisisitiza kuwa, Posta ni Taasisi pekee iliyo karibu na wananchi, na Serikali Inahitaji kuwafikia Wananchi wake , hivyo basi kupitia Posta, Serikali itaweza kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi.

 

Katika kukamilish Ziara yake , kiongozi huyo alitembelea Posta Kuu ya Dar e's Salaam (GPO) na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika ofisi hiyo ikiwemo kituo cha "Huduma pamoja".

 

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

 

 IMG 20210913 WA0085

Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao  (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi kuu za Shirika la Posta Tanzania na Kituo cha Huduma Pamoja jijini Dar es salaam. 
 
 
 
IMG 20210913 WA0044
 
Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania kabla ya kutembelea ofisi za Posta kuu na Kituo cha Huduma Pamoja jijini Dar es salaam.
 
 
 
 
IMG 20210913 WA0083
 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese kwa niaba ya Postamasta Mkuu, akizungumza wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao na Menejimenti ya Shirika la Posta, katika Makao Makuu ya Shirika , jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Isaac Gnamba Yao
 
 
 
 
 IMG 20210913 WA0081
 
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese (wa pili kushoto) Akitoa maelezo kwa niaba ya Postamasta Mkuu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao (kushoto) kuhusu mageuzi makubwa ambayo yamefanywa na Shirika katika utoaji huduma zake katika Ofisi Kuu ya Posta, jijini Dar es Salaam.
 
 
 
 
IMG 20210913 WA0080
 
Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Aron Samwel (kushoto aliyesimama) akitoa neno la shukrani mara baada ya kikao cha Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao na Menejimenti ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
 
 
 
 
IMG 20210913 WA0078
 
Baadhi ya Menejimenti ya Shirika la Posta wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao wakati wa kikao chake na Menejimenti hiyo kwenye Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania,  jijini Dar es salaam.
 
 
IMG 20210913 WA0076
 
Baadhi ya Menejimenti ya Shirika la Posta wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao wakati wa kikao chake na Menejimenti hiyo kwenye Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania,  jijini Dar es salaam.
 
 
 
 
IMG 20210913 WA0087
 
Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania mara baada ya kutembelea kituo cha Huduma pamoja katika Ofisi kuu ya Dar es Saam.
 
 
 
 IMG 20210913 WA0075
 
Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania mara baada ya ziara yake ya kutembelea kituo vya Huduma Pamoja, katika ofisi Kuu za Posta, jijini Dar es Salaam.
 
 
 
 
IMG 20210913 WA0073
 
Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Ivory Coast ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja Posta Afrika (PAPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao  (kushoto) akiagana na Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese (kwa niaba ya Kaimu Postamasta Mkuu) (wa tatu kulia) mara baada ya ziara yake katika ofisi kuu za Shirika hilo na Kituo cha Huduma Pamoja jijini Dar es salaam.

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!