KATIBU MKUU UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU) AWASILI JIJINI DODOMA

 
KATIBU MKUU UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU) AWASILI JIJINI DODOMA
 
IMG 20211008 WA0003
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja huo Bi. Jessica Ssengoba(katikati), na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania ndugu Macrice Daniel Mbodo.
 
 
 
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU),Bwana Sifundo Chief Moyo amewasili jijini Dodoma akiambatana na msaidizi wake Bi Jessica Uwera Ssengooba kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Siku Posta Duniani yatakayofanyika tarehe 9 Octoba, 2021. 
 
Maadhimisho hayo yametanguliwa na wiki ya maadhimisho ambapo shuguli mbalimbali zinafanyika kuanzia tarehe 6-9 Oktoba ,2021 na siku ya hitimisho ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango.
 
Katika ziara yake leo tarehe 7 Oktoba 2021 Ndg. Moyo amepata nafasi ya kumtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo na kufanya mazungumzo naye, pia ametembelea vituo vya Huduma Pamoja (One Stop Center) katika ofisi za Shirika hilo, jijini Dodoma. 
 
Akiwa ofisini hapo, ameeleza kuwa, Posta kwa sasa inaendelea kuboresha huduma zake na amempongeza Mwana Mbodo kwa juhudi anazoendelea kuzifanya katika kufanya magezi makubwa hasa yale yanayolifanya Shirika la POsta kuwa la Kidijitali. Ameongeza kuwa Shirika hilo linajiweka katika hatua nzuri kwani dunia imebadilika na mahitaji ya watu yanabadilika kulingana na mazingira
 
Aidha, Ndg. Moyo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Posta kuwa litaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kuifanya Sekta ya Posta kuwa ya kidijitali na yenye manufaa kwa jamii.
 
Naye Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo ameeleza kuwa Shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania linaendelea na mikakati yake ya kulifanya Shirika kuwa la kisasa zaidi kulingana na mahitaji ya wananchi wake, kwani tayari Serikali imeshawapatia  zaidi ya Bilioni 7 kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Shirika.
 
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu PAPU akiwa na msaidizi wake Jessica Ssengooba wameweza kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma likiwemo la Shirika la Posta na kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea katika ukumbi wa Jakaya kikwete, jijini Dodoma
 
Pia Katibu Mkuu huyo ameweza kushuhudia magari mapya yaliyonunuliwa na yatakabidhiwa kwa Shirika na mgeni Rasmi katika kilele cha siku ya Posta Dunia Oktoba 9,2021 Mheshimiwa Philip Isdor Mpango,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Katika ziara hiyo Kaimu Postamasta Mkuu aliambatana na  Mkuu cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Elia Madulesi, ambapo Viongozi wa PAPU waliambatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika ofisi ya Katibu Mkuu wa PAPU Bwana Amadou Bello.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
7 Octoba, 2021
 
 
 IMG 20211008 WA0069
 
 
IMG 20211008 WA0038
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika Posta Tanzania alipotembelea banda la maonesho la Shirika hilo Jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
 
 
 IMG 20211008 WA0068
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la Shirika hilo Jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
 
 
 
IMG 20211008 WA0060
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo( watatu kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na Postamasta Mkuu Mstaafu, Ndugu Deus Mndeme (wa pili kulia), Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu Macrice Mbodo (watatu kushoto), Naibu  Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Bi. Jessica Ssengooba(wa pili kushoto) na Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta, Ndugu Aron Samweli( wa kwanza kulia). 
 
 
IMG 20211008 WA0062
 Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo akishangilia jambo na Wafanyakazi wa Shirika Posta Tanzania alipotembelea banda la maonesho la Shirika hilo Jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
 
 
IMG 20211008 WA0070
 
 Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania ndugu Macrice Daniel Mbodo akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo katika pikipiki za Shirika la Posta kuelekea siku ya Posta duania Jijini Dodoma. 
 
 
IMG 20211008 WA0049
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo pamoja na mwenyeji wake Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania ndugu Macrice Daniel Mbodo  wakipata burudani ya nyimbo yenye ujumbe wa Posta kutoka kwa Mrisho Mpoto (Mjomba)
 
 
 IMG 20211008 WA0056
 
 Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo (kulia) na mwenyeji wake Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania ndugu Macrice Mbodo  (kushoto) wakishuhudia maonesho ya ngoma mbalimbali Jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
 
 
 IMG 20211008 WA0046
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ndugu Sifundo Chief Moyo (wa pili kulia) akiwa mbele ya magari ya shirika la posta Tanzania Jijini Dodoma. Watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja huo, Bi.Jessica Ssengooba, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Ndugu Macrice Mbodo,  na Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta, Ndugu Aron Samwel.
 
 
Top
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!