MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO AWA MGENI RASMI SIKU YA POSTA DUNIANI.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO AWA MGENI RASMI SIKU YA POSTA DUNIANI.
 
1 Isdor mpango
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.  
 
 
 
 
Tarehe 9 Oktoba 2021, 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango amekuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Posta Duniani, kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, Tanzania. 
 
 
Maadhimisho hayo yanayofanyika kila tarehe 8 na 9 Oktoba, yanaadhimishwa kwa mara ya 52 mwaka huu, huku yakiwa na kauli mbiu isemayo "Ubunifu kwa Posta Endelevu".
 
 
Katika hotuba yake, Dkt Mpango amepongeza mageuzi makubwa yanayofanyika ndani ya Shirika la Posta, huku akilisifu kwa kuleta huduma mbalimbali zinazoakisi matumizi ya teknolojia katika kuwahudumia Watanzania.  
 
 
"Tumeshuhudia Posta ikibadilisha namna ya utoaji huduma zake kulingana na mahitaji na ndio maana leo hii tunashudia hatua ya Posta kuwa ya kidigitali na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na kwa urahisi " alizungumza Dkt Mpango. 
 
 
Aidha, Dkt. Mpango aliongeza kuwa amefurahishwa na namna ambavyo kuna uhusiano kati ya malengo makuu ya Umoja wa Posta Duniani na malengo ya Taifa ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 na yale ya Sera ya Taifa ya Posta 2003 hasa katika kuwahudumia wananchi.
 
 
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amezungumzia umuhimu wa Shirika la Posta kwa jamii, huku akigusia ushindi wa Tanzania kwenye nafasi ya Ujumbe wa Baraza ya Utawala na Baraza la Uendeshaji la umoja wa Posta Duniani.
 
 
Nae Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Daniel Mbodo, amemshukuru Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, kwa kuwakabidhi magari 18 na Pikipiki 20 kwa ajili ya usafirishaji wa barua na vifurushi vya wateja, lengo likiwa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
 
 
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania. 
 
 
 
 
PICHA NA MATUKIO: 
 IMG 20211009 WA0052
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, ndugu Macrice Daniel Mbodo(wa pili kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika, Ndugu Sifundo Chief Moyo(wa pili kulia), katika maadhimisho ya siku ya Posta Duniani, kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
 
 
 
IMG 20211009 WA0056
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akijaribu moja ya gari ambalo amekabidhi kwa Shirika la Posta kama kitendea kazi cha usafirishaji wakati wa Maadhimisho ya siku ya Posta duniani.
 
 
 
IMG 20211009 WA0096
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari mapya yatakayotumiwa na shirika la Posta kusambaza barua na vifurushi vya wateja.
 
 
 
IMG 20211009 WA0089
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma. 
 
 
IMG 20211009 WA0101
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika, Ndugu Sifundo Chief Moyo akitoa salamu za Umoja wa Posta Afrika katika maadhimisho ya siku ya Posta Duniani Jijini Dodoma.
 
 
IMG 20211009 WA0068
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Ndugu Macrice Daniel Mbodo, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma. 
 
 
 
 
IMG 20211009 WA0083
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea taarifa za huduma za Posta katika banda la Shirika la Posta kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta, Ndugu Constantine Kasese (Kushoto).
 
 
 
IMG 20211009 WA0078
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhi cheti cha ushindi kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika shindano lililoendeshwa na Shirika la Posta Tanzania.
 
 
 
IMG 20211009 WA0115
 
Majeshi ya Ulinzi na usalama. 
 
 
 
IMG 20211009 WA0085
 
 Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. 
 
 
 
IMG 20211009 WA0114
 
 Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania akiskiliza jambo wakati wa maadhimisho hayo.
 
 
 
IMG 20211009 WA0102
 
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiskiliza jambo. 
 
 
 
IMG 20211009 WA0075
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Philip Mpango akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Shirika la Posta Tanzania. 
 
 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO: 
 
 
 
IMG 20211009 WA0066
 
 
 
IMG 20211009 WA0050
 
 
IMG 20211009 WA0076
 
 
IMG 20211009 WA0082
 
 
 
IMG 20211009 WA0065
 
 
IMG 20211009 WA0088
 
 
 IMG 20211009 WA0076
 
 
 
 
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!