POSTA YAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM

POSTA YAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM
 IMG 20211013 WA0120
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Mbodo (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof.Preksedis Ndomba.
 
 
 
 
Shirika la Posta Tanzania limeingia maakubaliano ya kibiashara na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) lengo likiwa ni kutatua changamoto na kuboresha mifumo ya TEHAMA ya Shirika la Posta Tanzania itakayowezesha urahisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
       
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Macrice Daniel Mbodo, alisema kuwa ushirikiano huu ni muendelezo wa mikakati ya Posta ya kusogeza huduma karibu na jamii kulingana na mahitaji yao
          
" Katika safari ya Posta huu ni muendelezo wa mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika katika uboreshaji wa huduma zake" Macrice Mbodo
             
Aidha, Kaimu Postamasta Mkuu ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wananchi kuwa, Posta inaendelea kuboresha huduma zake kwa kulifanya Shirika kuwa la kidijitali ili kuendana na mahitaji ya dunia ya sasa na kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi
 
 Naye, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof.Preksedis Ndomba alieleza kuwa Taasisi hizi zimewekwa ili kufikia na kutimiza mahitaji ya wananchi wake hivyo DIT imeingia makubaliano haya ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii ili kuleta tija kwa Taifa na kwa Taasisi hizi mbili
 
Prof. Preksedis aliongeza kuwa, kupitia mtandao mpana wa Shirika la Posta nchini DIT itaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia utoaji wa  elimu ya TEHAMA itakayokuwa inatolewa na Taasisi hiyo nchini
 
Makubaliano hayo ya kibiashara yamesainiwa leo tarehe 12 Oktoba, 2021 na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Macrice Mbodo pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo na kuhudhuriwa na Maafisa kutoka Shirika la Posta Tanzania pamoja na maafisha kutoka DIT, jijini Dar e's Salaam. 
 
 
Imetolewa na 
Ofisi ya Mawasiliano 
Shirika la Posta Tanzania 
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!