POSTA YASHIRIKI MKUTANO WA TEHAMA

 
 
POSTA YASHIRIKI MKUTANO WA TEHAMA
Mbodo 3
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Daniel Mbodo, akitoa wasilisho kuhusiana na Vituo vya Huduma Pamoja ndani ya Ofisi za Posta kwenye Mfumo Jumuishi, leo wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka TEHAMA wenye kauli mbiu "Kujenga Taifa la Kidijitali" kwenye ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha.
 
 
Kaimu Postamasta Mkuu alivyoshiriki Mkutano wa tano wa Mwaka wa TEHAMA unaoendeleo katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha
 
Mkutano huo wenye kauli mbiu #KujengaTaifaLaKidijitali ulianza rasmi tarehe 20 Octoba mwaka huu na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni Mwenyekiti ya mkutano huo
 
Aidha, mkutano huo umeambatana na maonesho mbalimbali ya watoa huduma za Mawasiliano ikiwemo Shirika la Posta nchini lengo ikiwa ni kutoa elimu na umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika Taifa na jamii endelevu
 
Imetolewa na,
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
21 Octoba, 2021.
 
#KujengaTaifaLaKidijitali
 
 
PICHA ZA TUKIO HILO: 
 
 
IMG 20211021 WA0029
 
IMG 20211021 WA0025
 
IMG 20211021 WA0018
 
IMG 20211021 WA0031
 
IMG 20211021 WA0035
 
IMG 20211021 WA0017
 
IMG 20211021 WA0020
 
IMG 20211021 WA0023
 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!