POSTA YAFANYA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA NA DSTV

POSTA YAFANYA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA NA DSTV
 
IMG 20211027 WA0046
 
 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Macrice Daniel Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo ya kibishara na Maafisa Biashara wa kampuni ya MultiChoice Tanzania maarufu kama DStv. 
 
Mazungunzo hayo yamefanyika leo tarehe 27 Oktoba, 2021 kwenye ukumbi wa Bodi uliopo gorofa ya 12 katika Makao Makuu ya Posta, jijini Dar es Salaam. 
 
Mkutano huo ulilenga kujadili namna ambavyo taasisi hizi mbili zitakavyowahudumia wananchi wengi zaidi na kwa haraka kupitia mtandao mpana ulioenea nchi nzima wa Shirika la Posta Tanzania.
 
Ujumbe kutoka Kampuni ya Multichoice Tanzania uliongozwa na Meneja Kitengo cha Bishara Bi. Enna Kiondo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara Bw. Eriq Mfinanga pamoja na Afisa Biashara wa Kampuni hiyo  Bw. Matoke matoke
 
Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Mameneja Wakuu wa Shirika la Posta nchini pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Shirika la Posta.
 
Imetolewa na,
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
27 Oktoba, 2021.
 
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!