POSTA YAKUTANA NA TSN

POSTA YAKUTANA NA TSN

567883A2 0D9B 43B8 A4DD 692727792C81

 

 

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo ya kibiashara na Uongozi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN katika Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2021, ulilenga kujadili namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana katika biashara pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi hasa katika nyanja za Usafirishaji wa magazeti, huduma za Uwakala kuuza magazeti, huduma za Uchapishaji (Printing) pamoja na eneo la matangazo (Publicity) ambapo kila Taasisi itanufaika na ushirikiano huo.

Ujumbe kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN uliongozwa na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo Bi.Tuma D. Abdallah akiambatana na Viongozi waandamizi wa Kampuni hiyo.

Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta nchini pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Shirika la Posta nchini

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano,

Shirika la Posta Tanzania.

28 Oktoba, 2021

 

PICHA NA MATUKIO 

D0F37E8E 5CF9 443C 8984 78C130CE8FBE

 Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Daniel Mbodo (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TSN mara baada ya mkutano. Kushoto aliyekaa ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya TSN Bi.Tuma D. Abdallah.

16D91C30 2467 494E 9B53 E936E4B5887D

 Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya TSN Bi.Tuma D. Abdallah akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kaimu Postamasta Mkuu mara baada ya kufika katika Makao Makuu ya Posta, jijini Dar es Salaam

01C2ACF9 8B52 43A6 B4E3 2B51DC77C0A1

 

399B61B1 110A 4779 BB27 077952E76BDB 

 

6E80DA48 2BC7 4F90 A148 62341CA00C54

 

 

38282E0A 4036 4E7A B504 A366A4B8CA9B

 

 

 

Tanzania Census 2022

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!