POSTA KUSHIRIKIANA NA EQUITY BANK

POSTA KUSHIRIKIANA NA

EQUITY BANK

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo ya kibiashara na Uongozi wa Benki ya Equity Tanzania, Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo uliofanyika leo tarehe 30 Oktoba, 2021, ulilenga kujadili namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana katika kutoa huduma za kibenki kwa wananchi kupitia mtandao mpana wa Posta ulionenea nchi nzima.

Aidha, kupitia mkutano huo taasisi hizo zimeweza kuelezea fursa mbalimbali zinazopatikana ili kuboresha na kurahisisha huduma kwa wananchi hasa katika nyanja za Duka Mtandao la Posta, huduma za uwakala na fedha pamoja na huduma za Usafirishaji

Kupitia huduma hizo kutafunguka fursa mbalimbali kwa mwananchi za kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha, urahisi wa malipo kwenye  mitandao, kwa upande wa Benki ya Equity wametaka Shirika la Posta litumie fursa hiyo kutoa huduma na Shirika litatoa huduma za Usafirishaji kwa Benki ya Equity ili kila Taasisi inufaike na ushirikiano huo.

Ujumbe kutoka Benki ya Equity uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Esther Kileo Kitoka akiambatana na Viongozi wengine waandamizi wa Benki hiyo.

Kwa upande wa Shirika la Posta Tanzania, mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Shirika.

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano,

Shirika la Posta Tanzania.

30 Oktoba, 2021.                  
                                                                  

E1DF7827 0580 4542 879E ECACCC128A33

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo (Kulia) akizungumza wakati wa mkutano na uongozi wa Benki ya Equity. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Esther Kileo Kitoka.

F4F3C5BD E608 4FC5 8C00 5E045BAF4765

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Esther Kileo Kitoka akizungumza wakati wa mkutano huo.

B600D806 85DB 43A4 AE90 80084D98F42A

 

7C6746D9 9DC5 43DA 99A6 398E2A2E0A6D


EDC83C63 9277 4AEC B2EC 61AA45ED8F30

Mkuu wa Kitengo cha Malipo ya Kidigitali Ralph J. Ligallama akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo.

5852BF31 EC9C 4F6D 9791 245688A0813D

 

4B6A4AE3 958D 4170 AF6E 09DCDBDEC8F7

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Equity Benki pamoja na Baadhi ya wajumbe Menejimenti ya Shirika la Posta nchini. Aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Esther Kileo Kitoka.

18082FDC 9766 48FB B0D3 C48376FB83A1

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!