📍MSAJILI WA HAZINA AFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU POSTAMASTA MKUU📍
MSAJILI WA HAZINA AFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU POSTAMASTA MKUU
Msajili wa Hazina Ndg. Mgonya Benedicto amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Mbodo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam
Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Kaimu Postamasta Mkuu Bwana Mbodo alipomtembelea Msajili wa Hazina ofisini kwake ikiwa ni ziara yenye lengo la kujenga uelewa wa safari ya Shirika la Posta Tanzania kwenye mazingira ya kidijitali. Itakumbukwa kuwa Msajili wa Hazina ndiye msimamizi wa Mashirika ya Umma likiwemo Shirika la Posta Tanzania.
Bwana Mbodo alipata nafasi ya kumfahamisha Msajili wa Hazina *Shirika la Posta lilipotoka, lilipo na mwelekeo wa Posta ya Kidijitali.*
Kwa upande wake Msajili wa Hazina Bwana Mgonya amepongeza mikakati na jitihada zinazoendelea kufanywa na Shirika la Posta Tanzania katika kuboresha utoaji wa huduma zake ndani na nje ya nchi yetu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania;
04 Novemba, 2021.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Mbodo (Kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Msajili wa Hazina Ndg. Mgonya Benedicto, katika ofisi za Msajili huyo jijini Darves Salaam
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Mbodo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Msajili wa Hazina Ndg. Mgonya Benedicto, jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja Msajili wa Hazina Ndg. Mgonya Benedicto (kulia) na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Mbodo (kushoto), mara baada ya kikao chao, jijini Dar es Salaam.