Tanzania Census 2022

📍POSTA YASHIRIKI TAMASHA LA DODOMA WINE FESTIVAL📍

POSTA YASHIRIKI TAMASHA LA DODOMA WINE FESTIVAL

Tarehe 6/11/2021,

Shirika la Posta Tanzania limeshiriki Tamasha la “ *Dodoma Wine Festival”,* ambalo limefanyika kwa siku nne mfululizo kuanzia tarehe 4 - 7 Novemba, 2021, jijini Dodoma.

Tamasha hilo limewakusanya wadau mbalimbali wanaofanya biashara tofauti tofauti katika kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la zabibu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb) alitembelea Banda la Shirika la Posta Tanzania na wakati wa Tamasha hilo Ili kujionea biashara na Huduma mbali mbali zinazofanywa na Shirika kama mdau katika mchakato wa kushiriki kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la zabibu.

Akitoa maelezo kwa Mhe Spika, Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dodoma Ndugu Ferdinand Kabyemela, alimueleza Spika wa Bunge kuwa Shirika ni mdau wa usafirishaji kwa kiasi kikubwa Shirika limejipanga kuhakikisha bidhaa za zabibu zinazozalishwa na viwanda mbalimbali nchini zinasafirishwa kwa uhakika, haraka na gharama nafuu hivyo kusaidia kukuza uchumi wa Taifa.

Bwana Kabyemela, aliongeza kuwa, Shirika kupitia Duka lake la mtandao limejipanga kuhakikisha bidhaa za zabibu zinazozalishwa nchini zinapata masoko duniani kote kwani duka hilo limeunganishwa na mtandao wa Umoja wa Posta Duniani hivyo kuwa na uwanda mpana wa wateja, kwani nchi zaidi ya mia moja na tisini na mbili ambazo ni wanachama wa umoja huo, zina uwezo wa kulifikia duka hilo moja kwa moja.

Kwa upande wake Mheshimiwa Spika, amelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa kuendelea na mageuzi ya kidijitali na hakusita kuonyesha kufurahishwa na jinsi mageuzi hayo yanavyochangia makundi mbali mbali ya kijamii kuweza kuhudumiwa ndani ya Shirika la Posta.

Katika ziara hiyo Mhe. Spika, aliambatana na wabunge Mhe. Dr. Charles Mwijage wa Jimbo la Muleba Kaskazini na Mhe. Dr. Oscar Kikoyo wa Jimbo la Muleba Kusini waliweza kutembelea banda la Shirika la Posta na kupata taarifa mbali mbali zihusuzo Shirika la Posta nchini.

 

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano,

Shirika la Posta Tanzania.

06 Novemba, 2021.

 

1C4006D0 35F1 42D3 85AF 04529CD975D4

F734B8D8 4C92 49DB 9356 7DDFB0CCAEFA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb) (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dodoma Ndugu Ferdinand Kabyemela (kulia) kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika, katika Tamasha la “ *Dodoma Wine Festival”, jijini Dodoma.

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!