Tanzania Census 2022

📍POSTA YAFANYA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA NA ATCL📍

POSTA YAFANYA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA NA ATCL

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Daniel Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo ya kibiashara na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ndg. Ladislaus Matindi katika ofisi za ATCL, leo jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna ambavyo taasisi hizi mbili zinavyoweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi hasa katika nyanja za usafirishaji wa mizigo, vifurushi na vipeto ndani na nje ya nchi pamoja na Ukataji wa tiketi za ndege kupitia mtandao wa posta ulioenea nchi nzima

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka Shirika la Posta Tanzania pamoja na Shirika la ndege Tanzania (ATCL)

 

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
08 Novemba, 2021.

174BFC24 0656 444A B9D9 95823FF0A3CF

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Daniel Mbodo akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ndg. Ladislaus Matindi, mara baada ya kikao hicho, jijini Dar es Salaam

CFD19E5D 9EEC 4F17 8B06 6B471638C7F2

0FFA2E23 BB31 49BB 8752 EEEA1E64C706

04FE431F 8527 4824 BCF3 E2B0EA934E9C

112FC7A5 0265 4923 87C9 C2649D4AFBBE

AA84E75C 3C35 4534 B7BC 2B2D5D72433D

97FBAF41 A2D5 4A10 A74C 45E0934C0EEA

 

 

 

X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!