📍POSTA YASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MASHUJAA WA VITA YA KWANZA YA DUNIA📍
POSTA YASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MASHUJAA WA VITA YA KWANZA YA DUNIA
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Constantine Kasese kwa niaba ya Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo Ndg. Macrice Daniel Mbodo, amehudhuria tukio la kuweka mashada katika makaburi ya Mashujaa waliopigana vita ya kwanza ya dunia kati ya mwaka 1914-1918 kama ishara ya kuwaenzi mashujaa hao,ijulikanayo kama #Layingwreathceremony# katika ofisi za Shirika la Posta zilizopo Posta ya zamani, jijini Dar es Salaam
Kumbukumbu hii huadhimishwa duniani kote kila siku jumapili ya mwanzo ya mwezi Novemba, ambapo mataifa mbalimbali hutumia hufanya ibada maalum, kuwaombea mashujaa hao pamoja kuweka mashada maalum katika makaburi yao
Kwa upande wa Tanzania tukio hili limeratibiwa na Jumuiya ya wanajeshi wastaafu waliopigana vita ya kwanza na ya pili ya dunia (The Tanzania Legion Club) na hufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam katika maeneo ya makumbusho, posta na katika maeneo mengine yenye makaburi hayo
Shirika la Posta Tanzania kama Taasisi ya mawasiliano iliyokuwepo tangu kipindi cha vita hizo imetunza kumbukumbu ya mashujaa hao kwa kuweka makaburi ya mashujaa hao katika ofisi zake za Sokoine zilizopo Posta ya zamani, jijini Dar es Salaam
Sambamba na hilo, Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara Ndg. Kasese alipata wasaa wa kuwakabidhi zawadi ya Stempu wageni waliofika katika ofisi za Shirika la Posta (Posta ya zamani) kama sehemu ya kumbukumbu kwao
Tukio hili limehudhuriwa na Meneja mkoa wa Shirika la Posta Tanzania, maafisa waandamizi wa Shirika hilo, wawakilishi kutoka ubalozi wa Uturuki, Mwambata wa Jeshi kutoka ubalozi huo, wawakilishi kutoka Jumuiya ya wanajeshi wastaafu (The Tanzania Legion Club) Mstaafu kutoka jeshi la Scotland pamoja na wawakilishi kutoka Jumuiya ya watanzania waliosoma nchini Uingereza.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
14 Novemba, 2021.